[10.4] Kwake Yeye tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadiya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiyealiye anzisha uumbaji, na kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walio amini na wakatendamema. Na walio kufuru, wao watapata vinywaji vinavyochemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru.
[10.15] Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana na Sisi husema: Lete Qur'ani isiyokuwa hii, au ibadilishe. Sema: Hainifalii mimi kuibadilisha kwa nitakavyo nafsi yangu. Mimi sifuatiila ninayo funuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi naogopa,nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu.
[10.22] Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini.Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda naokwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia,na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaonawamesha zongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwakumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru.
[10.24] Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama majituliyo yateremsha kutoka mbinguni, kishayakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu nawanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, naikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza,iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kamailiyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivitunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.
[10.61] Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemuyoyote katika Qur'ani, wala hamtendi kitendo chochoteila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnapo shughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenyeuzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu,wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika Kitabu kilicho wazi.
[10.71] Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake:Enyi watu wangu! Ikiwa kukaa kwangu nanyi nakukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungukunakutieni mashaka basi mimi namtegemea MwenyeziMungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikanekwenu. Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.