[11.7] Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katikasiku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu yamaji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Na weweukisema: Nyinyi hakika mtafufuliwa baada ya kufa; walewalio kufuru husema: Hayakuwa haya ila ni uchawi uliyo wazi.
[11.17] Basi je, mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Molawake Mlezi, inayo fuatwa na shahidi anaye toka kwake,na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema - hao wanamuamini, na anaye mkataakatika makundi, basi Moto ndio pahala pa miadi yao.Basi usiwe na shaka juu ya hayo. Hii ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi; lakini watu wengi hawaamini.
[11.31] Wala sikwambiini kuwa nina khazina za MwenyeziMungu; wala kuwa mimi najua mambo ya ghaibu; walasisemi: Mimi ni Malaika. Wala siwasemi wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapakheri - Mwenyezi Mungu anajua yaliomo katika nafsi zao- hapo bila ya shaka ninge kuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
[11.88] Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninayodalili wazi inayo tokana na Mola wangu Mlezi, na ikawaYeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayokukatazeni. Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza.Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. KwakeYeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea.