[12.31] Alipo sikia yule bibi masengenyo yao aliwaita, naakawawekea matakia ya kuegemea, na akampa kila mmojawao kisu. Akamwambia Yusuf: Tokeza mbele yao. Basi walipo mwona waliona ni kitu kikubwa kabisa, nawakajikata mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi! Huyusi mwanaadamu. Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu.
[12.80] Walipo kata tamaa naye wakenda kando kunong'ona.Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenuamechukua ahadi kwenu kutokana na Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo mlimkosa katika agano lenu juu ya Yusuf?Basi mimi sitotoka nchi hii mpaka baba yangu aniperuhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu.
[12.100] Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti chaenzi. Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewebaba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Na Mwenyezi Mungu ameijaalia iwe kweli. NaMwenyezi Mungu amenifanyia wema kunitoa gerezani, nakukuleteni kutoka jangwani baada ya Shet'ani kuchocheabaina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi niMpole kwa alitakalo. Bila ya shaka Yeye ni MjuziMwenye hikima.