[13.4] Na katika ardhi vimo vipande vilivyo karibiana, nazipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitendeyenye kuchipua kwenye shina moja na isio chipua kwenye shina moja, nayo inatiliwa maji yale yale. Natunaifanya baadhi yao bora kuliko mengine katika kula.Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanao tia mambo akilini.
[13.16] Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema:Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewebadala yake kuwa ni walinzi, nao hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuonahuwa sawa? Au hebu huwa sawa giza na mwangaza? Auwamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia?Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. NaYeye ni Mmoja Mwenye kushinda!
[13.17] Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabondeyakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafurikoyakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Nakutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutakamapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifanoya Haki na baat'ili. Basi lile povu linapita kamatakataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakiakwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo pigamifano.
[13.31] Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayoendeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewawafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali mambo yoteni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwambalau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shakaangeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkiakaribu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya MwenyeziMungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
[13.33] Je! Anaye isimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa nawashirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa khabari yayale asiyo yajua katika ardhi; au ni maneno matupu?Bali walio kufuru wamepambiwa vitimbi vyao nawamezuiliwa njia. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwachaapotee basi hana wa kumwongoa.