[14.9] Je! Hazikukufikieni khabari za walio kabla yenu?Kaumu ya Nuhu, na A'adi, na Thamud, na walio baadayao, ambao hapana awajuaye ila Mwenyezi Mungu? Mitumewao waliwajia kwa hoja zilizo wazi, na wao wakarudishamikono yao kwenye vinywa vyao, wakasema: Hakika sisitumeyakataa hayo mliyo tumwa, na hakika sisi tuna shaka kubwa na mnayo tuitia.
[14.10] Mitume wao wakasema: Ati pana shaka na MwenyeziMungu, Muumba mbingu na ardhi? Yeye anakuiteni apatekukufutieni madhambi yenu, na akupeni muhula mpaka muda ulio wekwa. Wakasema: Nyinyi si chochote ila niwanaadamu kama sisi. Mnataka kutuzuilia na waliyo kuwawakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni hoja ilio wazi.
[14.21] Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu.Wanyonge watawaambia walio takabari: Sisi tulikuwawafwasi wenu; basi hebu hamtuondolei kidogo hivikatika adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: LauMwenyezi Mungu angeli tuongoa basi hapana shaka nasitungeli kuongoeni. Ni mamoja kwetu tukipapatika autukisubiri; hatuna pa kukimbilia.
[14.22] Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: HakikaMwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Naminalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa namamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyimkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, walanyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika miminilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu.