Skip to Content
The Muslims Internet Directory
Featured Service
Home
|
Advertise
|
FAQ
|
Login/Register |
Directory
Quran
Hadith
Islamic Library
Prayer Times
Discover Islam
Islamic Gallery
Calendar
New
Classifieds
Services
Webmasters
Dictionary
Downloads
Kids & Games
Quran Navigation
Search
Translations
Transliteration
Index
Chapter Info
English Search
Articles and Books
Audio
Memorization
Links
Downloads
On Your Site
FAQ
Muslims Internet Directory
The Quran / English
The Hadith
2Muslims.com
Our Network
Islamic Library & Articles
The Internet
Islamic Classifieds
WebRing Members Sites
Advance
-
Live Search
-
Quran
-
Hadith
-
Search This Site
-
The Network
-
Classifieds
-
WebRing
-
The Internet
-
Help!
Featured Site
Feature Your Site Now
2Muslims Services
Islamic IE Toolbar
Islamic Internet Gadgets
Prayer Times Software
Forum
Donate
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Polls
Free E-mail Account
Zakat Calculator
Islamic Holidays Dates
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Buy The Islamic CD
God's Attributes
How To Pray?
Paid Services
Buy The Islamic CD
Banner Design
Submit Your Site
Muslims Million Pixels
Translate Site To:
Arabic
Bulgarian
Catalan
Chinese (Simplified)
Chinese (Traditional)
Croatian
Czech
Danish
Dutch
English
Filipino
Finnish
French
German
Greek
Hebrew
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latvian
Lithuanian
Norwegian
Polish
Portuguese
Romanian
Russian
Serbian
Slovak
Slovenian
Spanish
Swedish
Ukrainian
Vietnamese
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
view results
view other polls
Home
:
Quran:
Quran Translations:
Swahili:
SURA AL ISRAAI :
Search the Quran in any of the drop down menu languages:
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Chinese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
More search options
SURA AL ISRAAI
[17.1] SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usikummoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali,ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye niMwenye kusikia na Mwenye kuona.
[17.2] Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya uwongofu kwaWana wa Israili. (Tukawambia): Msiwe na mtegemewa ilaMimi!
[17.3] Enyi kizazi tuliyo wachukua pamoja na Nuhu! Hakikayeye alikuwa mja mwenye shukrani.
[17.4] Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabukwamba: Hakika nyinyi mtafanya fisadi katika nchi marambili, na kwa yakini mtapanda kiburi, kiburi kikubwa.
[17.5] Basi itapo fika ahadi ya kwanza yaketutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwaahadi iliyo timizwa.
[17.6] Kisha tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao, natukakusaidieni kwa mali na wana, na tukakujaalienimkawa wengi zaidi.
[17.7] Basi mkifanya wema, mnajifanyia wema nafsi zenu. Namkifanya ubaya, mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadiya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza,na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.
[17.8] Huenda Mola wenu Mlezi akakurehemuni. Na mkirudiana Sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannamu kuwa nigereza kwa ajili ya makafiri.
[17.9] Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyookakabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda memaya kwamba watapata malipo makubwa.
[17.10] Na yakwamba wale wasio iamini Akhera tumewaandaliaadhabu chungu.
[17.11] Na mwanaadamu huomba shari kama vile aombavyokheri, kwani mwanaadamu ni mwenye pupa.
[17.12] Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili.Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya isharaya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi yamiaka na hisabu. Na kila kitu tumekifafanua waziwazi.
[17.13] Na kila mtu tumemfungia a'mali yake shingonimwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakachokikuta kiwazi kimekunjuliwa.
[17.14] Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yakoinakutosha leo kukuhisabu.
[17.15] Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsiyake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yakemwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.
[17.16] Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha walewenye starehe na taanusi, lakini wao huendelea kutendamaovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa.
[17.17] Na kaumu ngapi tumeziangamiza baada ya Nuhu! NaMola wako Mlezi anatosha kabisa kuwa ni Mwenye kuzijuana kuziona dhambi za waja wake.
[17.18] Anaye taka yapitayo upesi upesi, tutafanya harakakumletea hapa hapa tunayo yataka kwa tumtakaye. Kishatumemwekea Jahannamu; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa.
[17.19] Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudia'mali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yaoitakuwa ni ya kushukuriwa.
[17.20] Wote hao tunawakunjulia - hawa na hao - katikaneema za Mola wako Mlezi. Wala neema za Mola wakoMlezi hazizuiliki.
[17.21] Angalia vipi tulivyo wafadhili baadhi yao kulikowenginewe. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwazaidi na fadhila kubwa zaidi.
[17.22] Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu,usije ukawa wa kulaumiwa uliye tupika.
[17.23] Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabuduyeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Nasema nao kwa msemo wa hishima.
[17.24] Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaoneahuruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kamawalivyo nilea utotoni.
[17.25] Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu.Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenyekuwaghufiria wanao tubia kwake.
[17.26] Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, namsafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo.
[17.27] Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet'ani. NaShet'ani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi.
[17.28] Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehemaya Mola wako Mlezi unayo itaraji, basi sema nao manenolaini.
[17.29] Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwashingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabakiukilaumiwa muflisi.
[17.30] Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia rizikiamtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa wajawake ni Mwenye kuwajua na kuwaona.
[17.31] Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini.Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao nikhatia kubwa.
[17.32] Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu nanjia mbaya.
[17.33] Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekatazaisipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwabasi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.
[17.34] Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwanjia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeniahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa.
[17.35] Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizanizilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na khatimaye ndiobora.
[17.36] Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakikamasikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa.
[17.37] Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakikawewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wamilima.
[17.38] Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Molawako Mlezi.
[17.39] Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wakoMlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungumwengine, usije ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwana kufurushwa.
[17.40] Je! Mola wenu Mlezi amekuteulieni wavulana, naYeye akawafanya Malaika ni banati zake? Kwa hakikanyinyi mnasema usemi mkubwa.
[17.41] Na tumekwisha bainisha katika Qur'ani hii iliwapate kukumbuka. Lakini haikuwazidisha ila kuwa mbalinayo.
[17.42] Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungumingine kama wasemavyo, basi wangeli tafuta njia yakumfikia Mwenye Kiti cha Enzi.
[17.43] Subhanahu Wa Taa'la, Ametakasika na Ametukuka juukabisa na hayo wanayo yasema.
[17.44] Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyoteviliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwasifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira.
[17.45] Na unapo soma Qur'ani tunaweka baina yako na walewasio iamini Akhera pazia linalo wafunika.
[17.46] Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasijewakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Naunapo mtaja katika Qur'ani Mola wako Mlezi peke yake,basi wao hugeuka nyuma wakenda zao.
[17.47] Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayo sikiliziawanapo kusikiliza, na wanapo nong'ona. Wanapo sema haomadhaalimu: Nyinyi hamumfuati isipo kuwa mtu aliye rogwa.
[17.48] Tazama vipi wanavyo kupigia mifano. Basiwamepotea. Kwa hivyo hawawezi kuipata njia.
[17.49] Na walisema: Je! Tutapo kuwa mifupa na mapandeyaliyo vurugika, tutafufuliwa kwa umbo jipya?
[17.50] Sema: Kuweni hata mawe na chuma.
[17.51] Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifuavyenu. Watasema: Nani atakaye turudisha tena? Sema:Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisiavichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saayakawa karibu!
[17.52] Siku atakapo kuiteni, na nyinyi mkamuitikia kwakumshukuru, na mkadhani kuwa hamkukaa ila muda mdogotu.
[17.53] Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maanaShet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet'anini adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.
[17.54] Mola wenu Mlezi anakujueni vilivyo. Akipendaatakurehemuni, na akipenda atakuadhibuni. Nahatukukutuma ili uwe mlinzi juu yao.
[17.55] Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomombinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilishabaadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi.
[17.56] Sema: Waombeni hao mnao wadaia badala yake Yeye.Hawawezi kukuondoleeni madhara, wala kuyaweka pengine.
[17.57] Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia yakwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao waliokaribu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaakutahadhari nayo.
[17.58] Na hapana mji wowote ila Sisi tutauteketeza kablaya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Hayayamekwisha andikwa katika Kitabu.
[17.59] Na hapana kinacho tuzuia kupeleka miujiza ila nikuwa watu wa zamani waliikanusha. Na tuliwapaWathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri, lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatupeleki Ishara ilakwa ajili ya kuhadharisha.
[17.60] Na tulipo kwambia: Hakika Mola wako Mleziamekwisha wazunguka hao watu. Na hatukuifanya ndototulio kuonyesha ila ni kuwajaribu watu, na mti uliolaaniwa katika Qur'ani. Na tunawahadharisha, lakinihaiwazidishii ila uasi mkubwa.
[17.61] Na pale tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam.Wakamsujudia isipo kuwa Iblisi. Akasema: Je!Nimsujudie uliye muumba kwa udongo?
[17.62] Akasema: Hebu nambie khabari ya huyu uliye mtukuzajuu yangu. Ukiniakhirisha mpaka Siku ya Kiyama, hapanashaka nitawaangamiza dhuriya zake wasipo kuwa wachache tu.
[17.63] Akasema Mwenyezi Mungu: Ondokelea mbali! Atakayekufuata katika wao, basi Jahannamu itakuwa ndiyomalipo yenu, malipo ya kutimia.
[17.64] Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako,na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendaokwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shet'ani hawapi ahadi ila ya udanganyifu.
[17.65] Hakika wewe huna mamlaka juu ya waja wangu. NaMola wako Mlezi anatosha kuwa ni wa kutegemewa.
[17.66] Mola wenu Mlezi ndiye anaye kuendesheeni marikebukatika bahari ili mtafute katika fadhila zake. HakikaYeye ni Mwenye kukurehemuni nyinyi.
[17.67] Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnaowaomba wanapotea, isipo kuwa Yeye tu. Na anapo kuvuenimkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanaadamu ni mwingi wa kukanusha.
[17.68] Je! Mmeaminisha ya kuwa hatakudidimizeni upandewowote katika nchi kavu, au kwamba hatakuleteenitufani la kokoto? Kisha msipate wa kumtegemea.
[17.69] Au mmeaminisha ya kuwa hatakurudisheni humo maranyengine na kukupelekeeni kimbunga cha upepoakakuzamisheni kwa mlivyo kufuru, na kisha msipate wa kukunusuruni nasi.
[17.70] Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vyakupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vituvizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.
[17.71] Siku tutapo waita kila kikundi cha watu kwa mujibuwa wakifuatacho - basi atakaye pewa kitabu chake kwamkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao wala hawatadhulumiwa hata chembe.
[17.72] Na aliye kuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofuAkhera, na atakuwa aliye ipotea zaidi Njia.
[17.73] Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyokufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangelikufanya rafiki.
[17.74] Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibiakuwaelekea kidogo.
[17.75] Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabumardufu ya uhai, na adhabu mardufu ya kifo. Kishausinge pata mtu wa kukunusuru nasi.
[17.76] Na walitaka kukukera ili uitoke nchi. Na hapo waowasingeli bakia humo ila kwa muda mchache tu.
[17.77] Huo ndio mwendo kwa Mitume tulio watuma kablayako. Wala hupati mabadiliko katika mwendo wetu.
[17.78] Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku,na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiriinashuhudiwa daima.
[17.79] Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya sunna khasakwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheokinacho sifika.
[17.80] Na sema: Mola wangu Mlezi! Niingize muingizomwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazotoka kwako zinisaidie.
[17.81] Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka.Hakika uwongo lazima utoweke!
[17.82] Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabuna rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimuila khasara.
[17.83] Na mwanaadamu tunapo mneemesha hugeuka nakujitenga kando. Na inapo mgusa shari hukata tamaa.
[17.84] Sema: Kila mmoja anafanya kwa namna yake. Na Molawenu Mlezi anajua aliye ongoka katika njia.
[17.85] Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho nikatika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewakatika ilimu ila kidogo tu.
[17.86] Na tungeli penda tungeli yaondoa tuliyo kufunulia.Kisha usingeli pata mwakilishi wa kukupigania kwetukwa haya.
[17.87] Isipo kuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi.Hakika fadhila yake kwako ni kubwa.
[17.88] Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili waletemfano wa hii Qur'ani basi hawaleti mfano wake, hatawakisaidiana wao kwa wao.
[17.89] Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur'ani kwakila mfano. Lakini watu wengi wanakataa isipo kuwakukanusha tu.
[17.90] Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbuliechemchem katika ardhi hii.
[17.91] Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, nautupitishie mito kati yake ikimiminika.
[17.92] Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai; au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwauso.
[17.93] Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni.Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabutukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu naMtume?
[17.94] Na nini kilicho wazuilia watu kuamini ulipo wajiauwongofu isipo kuwa walisema: Je! Mwenyezi Munguhumtuma mwanaadamu kuwa ni Mtume?
[17.95] Sema: Ingeli kuwa duniani wapo Malaika wanatembeakwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao.
[17.96] Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi bainayangu na nyinyi. Hakika Yeye anawajua vyema waja wakena anawaona.
[17.97] Na anaye mhidi Mwenyezi Mungu basi huyo ndiyealiye hidika. Na anaye wapotoa basi huto wapatiawalinzi badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyamahali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu namabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kilamoto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwanguvu.
[17.98] Hayo ni malipo yao kwa sababu walizikataa isharazetu, na wakasema: Hivyo tukisha kuwa mifupa namapande yaliyo vurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya?
[17.99] Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfanowao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhaalimu hawataki ila ukafiri.
[17.100] Sema: Lau kuwa nyinyi mnazimiliki khazina zarehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngelizuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu. Na mwanaadamu tangu hapo tabia yake ni mchoyo!
[17.101] Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizowazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, naFirauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musaumerogwa!
[17.102] Musa akasema: Wewe unajua bila ya shaka kuwa hayahakuyateremsha ila Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ilikuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwishaangamia.
[17.103] Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwahivyo tukamzamisha yeye na walio kuwa pamoja nayewote.
[17.104] Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili: Kaenikatika nchi. Itapo kuja ahadi ya Akhera tutakuleteninyote pamoja.
[17.105] Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Hakiimeteremka. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri namwonyaji.
[17.106] Na Qur'ani tumeigawanya sehemu mbali mbali iliuwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogokidogo.
[17.107] Sema: Iaminini au msiiamini. Hakika wale waliopewa ilimu kabla yake, wanapo somewa hii, huangukakifudifudi wanasujudu.
[17.108] Na wanasema: Subhana Rabbina, Ametakasika Molawetu Mlezi! Hakika ahadi ya Mola wetu Mlezi lazimaitimizwe!
[17.109] Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, nainawazidisha unyenyekevu.
[17.110] Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), aumwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolotemnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Walausitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifichekwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati yahizo.
[17.111] Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za MwenyeziMungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katikaufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.
Featured Ad
About Us
Contact Us
Advertise
Donate
Bookmark Us
Support Us
GuestBook
Link To Us
Newsletter
Recommend
Set as Home
Terms Of Use
What's New
Other Sites:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Pharmacy Site
-
Links SQL Plugins
This Page Was Last Updated on
Copyright 2003-2008
Islamic Education & Services Institute