[18.17] Na unaliona jua linapo chomoza linainamia kulianimwao kutoka hapo pangoni; na linapo kuchwa linawakwepakushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Ambaye MwenyeziMungu anamwongoa basi huyo ni mwenye kuongoka. Naanaye muacha kupotea basi hutampatia mlinzi wala mwongozi.
[18.19] Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapatekuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao:Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja ausehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi anajua zaidimuda mlio kaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedhazenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilichobora kabisa akuleteeni cha kukila. Naye afanye mambohayo kwa busara, wala asikutajeni kabisa kwa yeyote.
[18.21] Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapatekujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli,na kwamba Saa haina shaka. Walipo kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema: Jengeni jengo juu yao.Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shindakatika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao.
[18.22] Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao.Na wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.Wanavurumisha ovyo. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: Mola wangu Mlezindiye anaye jua sawa sawa hisabu yao. Hawawajui ilawachache tu. Basi usibishane juu yao ila kwa mabishanoya juu juu tu hivi. Wala usiulize khabari zao kwayeyote yule.
[18.29] Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi.Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisitumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama khema. Na wakiomba msaadawatasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka.Yatayo wababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno!Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno!
[18.57] Na ni nani dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuzana akasahau yaliyo tangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao iliwasifahamu, na uziwi kwenye masikio yao. Na ukiwaitakwenye uwongofu hawakubali kabisa kuongoka.
[18.82] Na ama ukuta, huo ulikuwa ni wa vijana wawilimayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako khazinayao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazinayao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola wakoMlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyondiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuwezakuyasubiria.