[22.5] Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwabasi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo,kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana nakipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo,ili tukubainishieni. Nasi tunakiweka katika matumbo yauzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kishatunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikiekutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, nawapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri waunyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwaanakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakinitunapo yateremsha maji juu yake husisimka nakututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri.
[22.18] Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Munguviliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, namwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu.Na anaye fedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wakumhishimu. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda apendayo.
[22.36] Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa nikudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; kwa hao mnakheri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanapo simama kwa safu. Na waangukapo ubavukuleni katika hao na walisheni walio kinai na wanaolazimika kuomba. Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru.
[22.40] Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki,ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni MwenyeziMungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba zawat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti,ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwawingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yuleanaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenyenguvu Mtukufu.
[22.78] Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kamainavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Walahakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu)alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii(Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, nanyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala natoeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeyendiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizibora kabisa.