[24.21] Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Naatakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrishamachafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingelitakasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. LakiniMwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, na Mwenyezi Munguni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
[24.31] Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao,na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri waoisipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwawaume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, auwatoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, auwana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawakewenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, auwafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambaohawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chinimiguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Natubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ilimpate kufanikiwa.
[24.33] Na wajizuilie na machafu wale wasio pata chakuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhilayake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambaomikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikienikama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali yaMwenyezi Mungu aliyo kupeni. Wala msiwashurutishevijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta patola maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujihishimu.Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani MwenyeziMungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[24.35] Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfanowa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yaketaa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafutayanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wamashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu yaNuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yakeamtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
[24.43] Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukumamawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi?Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe,akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye.Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho.
[24.55] Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio aminimiongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanyamakhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifawa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yaoaliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada yakhofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada yahayo, basi hao ndio wapotovu.
[24.58] Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyowamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighimiongoni mwenu mara tatu - kabla ya Sala ya alfajiri,na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada yaSala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu.Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo MwenyeziMungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu niMjuzi Mwenye hikima.
[24.61] Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru,wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkilakatika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za kaka zenu, au nyumba zadada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba zashangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba zadada wa mama zenu, au za mlio washikia funguo zao, aurafiki yenu. Si vibaya kwenu mkila pamoja au mbalimbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu,kuwa ni maamkio yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, yenyebaraka na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyokubainishieni Aya zake mpate kuelewa.
[24.62] Hakika Waumini wa kweli ni walio muamini MwenyeziMungu na Mtume wake; na wanapo kuwa pamoja naye kwajambo la kuwakhusu wote hawaondoki mpaka wamtake ruhusa. Kwa hakika wale wanao kuomba ruhusa, hao ndiowanao muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Nawakikuomba ruhusa kwa baadhi ya kazi zao, mruhusu umtakaye miongoni mwao, uwaombee msamaha kwa MwenyeziMungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe,Mwenye kurehemmu.