The Muslims Internet Directory
SURAT AL FURQAN
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT AL FURQAN
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[25.1] Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, iliawe mwonyaji kwa walimwengu wote.
[25.2] Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, walahakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katikaufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwakipimo.
[25.3] Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbichochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii nafsi zaomadhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai,wala kufufuka.
[25.4] Na wamesema walio kufuru: Haya si chochote ila niuzushi alio uzua, na wamemsaidia kwa haya watuwengine! Hakika hawa wamekuja na dhulma na uwongo.
[25.5] Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyoviandikisha, anavyo somewa asubuhi na jioni.
[25.6] Sema: Ameyateremsha haya ajuaye siri za katikambingu na ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenyekurehemu.
[25.7] Na wakasema: Ana nini Mtume huyu? Anakula chakula,na anatembea masokoni! Mbona hakuteremshiwa Malaikaakawa mwonyaji pamoja naye?
[25.8] Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa nabustani ale katika hiyo? Wakasema madhaalimu: Nyinyihamumfuati ila mtu aliye rogwa.
[25.9] Tazama jinsi wanavyo kupigia mifano. Basiwamepotea, wala hawataiweza Njia.
[25.10] Ametukuka ambaye akitaka atakujaalia yaliyo borakuliko hayo, nayo ni mabustani yapitayo mito kati yao,na atakujaalia majumba ya fakhari.
[25.11] Bali wanaikanusha Saa (ya Kiyama). Na Sisitumemuandalia Moto mkali kabisa huyo mwenye kuikanushaSaa..
[25.12] Ule Moto ukiwaona tangu mahali mbali wao watasikiahasira yake na mngurumo wake.
[25.13] Na watakapo tupwa humo mahali dhiki, haliwamefungwa, wataomba wafe.
[25.14] Msiombe kufa mara moja tu, bali mfe mara nyingi!
[25.15] Sema: Je! Haya ni bora au Pepo ya milele, ambayowameahidiwa wachamngu, iwe kwao malipo na marejeo?
[25.16] Watayapata humo wayatakayo daima dawamu. Hii niahadi juu ya Mola wako Mlezi, inayo ombwa.
[25.17] Na siku atakapo wakusanya wao na hao wanaowaabudu, na akasema: Je! Ni nyinyi mlio wapoteza wajawangu hawa, au wao wenyewe walipotea njia?
[25.18] Watasema: Subhanak, Umetakasika na upungufu!Haikutupasia sisi kuchukulia walinzi badala yako,lakini Wewe uliwastarehesha wao na baba zao hatawakasahau kukumbuka, na wakawa watu walio angamia.
[25.19] Basi walikukanusheni kwa mliyo yasema. Kwa hivyohamwezi kujiondolea wala kujisaidia. Na atakayedhulumu miongoni mwenu tutamwonjesha adhabu kubwa.
[25.20] Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwahakika na yakini walikuwa wakila chakula, na wakendamasokoni. Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni majaribio kwa wengine; je! Mtasubiri? Na Mola wakoMlezi ni Mwenye kuona.
[25.21] NA WALISEMA wale wasio taraji kukutana nasi: Mbonasisi hatuteremshiwi Malaika au hatumwoni Mola wetuMlezi? Kwa yakini hawa wamejiona bora nafsi zao, na wamepanda kichwa vikubwa mno!
[25.22] Siku watakayo waona Malaika haitakuwa furaha sikuhiyo kwa wakosefu. Na watasema: Mungu apishe mbali!
[25.23] Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendovyao, tuvifanye kama mavumbi yaliyo tawanyika.
[25.24] Watu wa Peponi siku hiyo watakuwa katika makaazibora na mahali penye starehe nzuri.
[25.25] Na siku zitapo funguka mbingu kwa mawingu, nawateremshwe Malaika kwa wingi,
[25.26] Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman,Mwingi wa Rehema, na itakuwa siku ngumu kwa makafiri.
[25.27] Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikonoyake, na huku anasema: Laiti ningeli shika njia pamojana Mtume!
[25.28] Ee Ole wangu! Laiti nisingeli mfanya fulani kuwarafiki!
[25.29] Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwishanijia, na kweli Shet'ani ni khaini kwa mwanaadamu.
[25.30] Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi!Hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni kihame.
[25.31] Na vivi hivi tumemfanyia kila Nabii adui miongonimwa wakosefu, na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenyekuongoa na Mwenye kunusuru.
[25.32] Na wakasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwaQur'ani kwa jumla moja? Hayo ni hivyo ilituuthibitishe moyo wako, na ndio tumeisoma kwamafungu.
[25.33] Wala hawatakuletea mfano wowote, ila na Sisitutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora.
[25.34] Wale ambao watakao kusanywa na kubururwakifudifudi mpaka kwenye Jahannamu, hao watakuwa namahali pabaya, ndio wenye kuipotea sana njia.
[25.35] Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukamweka pamojanaye nduguye, Harun, kuwa waziri.
[25.36] Tukawaambia: Nendeni kwa watu walio kanusha Isharazetu. Basi tukawateketeza kabisa.
[25.37] Na watu wa Nuhu, walipo wakanusha Mitume,tuliwazamisha, na tukawafanya ni Ishara kwa watu. Natumewaandalia wenye kudhulumu adhabu chungu.
[25.38] Na tuliwaangamiza kina A'di na Thamudi na watu waRass na vizazi vingi vilivyo kuwa kati yao.
[25.39] Na wote tuliwapigia mifano, na wote tuliwaangamizakabisa kabisa.
[25.40] Na kwa yakini wao wanafika kwenye nchi ilioteremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiiona?Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa.
[25.41] Na wanapo kuona hawakuchukulii ila ni mzaha tu, na(wanasema): Ati ndiye huyu Mwenyezi Mungu aliye mtumakuwa Mtume?
[25.42] Kwa hakika alikuwa karibu kutupoteza tuiachemiungu yetu, ingeli kuwa hatukushikamana nayo kwakuvumilia. Bado watakuja jua, watakapo iona adhabu, ninani aliye potea njia.
[25.43] Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwandio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?
[25.44] Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia auwanaelewa? Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, baliwao wamepotea zaidi njia.
[25.45] Je! Huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyo kitandazakivuli. Na angeli taka angeli kifanya kikatulia tu.Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.
[25.46] Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo.
[25.47] Naye ndiye aliye kufanyieni usiku kuwa ni vazi, nausingizi kuwa mapumziko, na akakufanyieni mchana nikufufuka.
[25.48] Naye ndiye anaye zituma pepo kuwa bishara njemakabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutokambinguni maji safi.
[25.49] Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyo kufa, natuwanyweshe wanyama na watu wengi tulio waumba.
[25.50] Na kwa yakini tumeisarifu kati yao wapatekukumbuka. Lakini watu wengi wanakataa ila kukufuru.
[25.51] Na tungeli taka tungeli peleka katika kila mjiMwonyaji.
[25.52] Basi usiwat'ii makafiri. Na pambana nao kwayo kwaJihadi kubwa.
[25.53] Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamumno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yaokinga na kizuizi kizuiacho.
[25.54] Naye ndiye aliye muumba mwanaadamu kutokana namaji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji. Na Molawako Mlezi ni Muweza.
[25.55] Na wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyowafaa wala yasiyo wadhuru. Na kafiri daima ni msaidiziwa kumpinga Mola wake Mlezi.
[25.56] Nasi hatukukutuma ila kuwa ni Mbashiri naMwonyaji.
[25.57] Sema: Sikukuombeni ujira juu yake; ila atakaye naashike njia iendayo kwa Mola wake Mlezi.
[25.58] Na mtegemee Aliye Hai, ambaye hafi. Na umtukuzekwa sifa zake. Na yatosha kwake kuwa yeye ni Mwenyekhabari za dhambi za waja wake.
[25.59] Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndaniyake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi,Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye.
[25.60] Na wanapo ambiwa: Msujudieni Arrahman! Wao husema:Ni nani Arrahman? Je! Tumsujudie unaye tuamrisha wewetu? Na huwazidishia chuki.
[25.61] Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, naakajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara.
[25.62] Naye ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatanakwa nafuu ya anaye taka kukumbuka, au anaye takakushukuru.
[25.63] Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemezahujibu: Salama!
[25.64] Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezikwa kusujudu na kusimama.
[25.65] Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondoleeadhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtuhaimwachi.
[25.66] Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya.
[25.67] Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo walahawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina yahayo.
[25.68] Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja naMwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimishaMwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - naatakaye fanya hayo atapata madhara,
[25.69] Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumuhumo kwa kufedheheka.
[25.70] Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatendavitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilishamaovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[25.71] Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyoametubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu.
[25.72] Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uwongo, na pindiwapitapo penye upuuzi, hupita kwa hishima yao.
[25.73] Na wale ambao wanapo kumbushwa Ishara za Mola waoMlezi hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu.
[25.74] Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe katikawake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalietuwe waongozi kwa wachamngu.
[25.75] Hao ndio watakao lipwa makao ya juu kwa kuwawalisubiri, na watakuta humo maamkio na salamu.
[25.76] Wadumu humo - kituo na makao mazuri kabisa.
[25.77] Sema: Mola wangu Mlezi asinge kujalini lau kuwa sikuomba kwenu. Lakini nyinyi mmemkadhibisha. Basiadhabu lazima iwe.
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN