[28.15] Na akaingia mjini wakati wa kughafilika wenyejiwake, na akakuta humo watu wawili wanapigana - mmojani katika wenzake, na mwengine katika maadui zake. Yule mwenzake alimtaka msaada kumpiga adui yake. Musaakampiga ngumi, akamuuwa. Akasema: Hiki ni kitendo chaShet'ani; hakika yeye ni adui, mpotezaji dhaahiri.