[29.10] Na katika watu wapo wanao sema: TumemuaminiMwenyezi Mungu. Lakini wanapo pewa maudhi kwa ajili yaMwenyezi Mungu, wanayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapo kuja nusura kutokakwa Mola wako Mlezi husema: Hakika sisi tulikuwapamoja nanyi. Kwani Mwenyezi Mungu hayajui yaliomo vifuani mwa walimwengu?
[29.40] Basi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosayake. Kati yao wapo tulio wapelekea kimbunga chachangarawe; na kati yao wapo walio nyakuliwa naukelele; na kati yao wapo ambao tulio wadidimizakatika ardhi; na kati yao wapo tulio wazamisha. WalaMwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakiniwalikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao.