[34.3] Na walisema walio kufuru: Haitatufikia Saa (yaKiyama). Sema: Kwani? Hapana shaka itakufikieni, naapakwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinacho fichikana kwake hata chenye uzito wachembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, walakilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi; ila vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenyekubainisha.
[34.12] Na Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safariyake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safariyake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Natukamyayushia chemchem ya shaba. Na katika majiniwalikuwako walio kuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamwonjesha adhabuya Moto unao waka.
[34.33] Na wanyonge wakawaambia walio takabari: Bali nivitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipo kuwamkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika. Nao wataficha majuto watakapo iona adhabu.Na tutaweka makongwa shingoni mwao walio kufuru. Kwaniwanalipwa ila kwa waliyo kuwa wakiyatenda?