[35.11] Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo.Kisha kwa tone la manii. Kisha akakufanyeni mwanamumena mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, ila kwa ilimu yake. Na wala hapewi umrimwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake,ila yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.
[35.18] Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Na aliyetopewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe hautachukuliwahata kidogo, na angamwomba jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu,na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasakwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.