[40.28] Na akasema mtu mmoja Muumini, aliye kuwa mmojakatika watu wa Firauni aliye ficha Imani yake:Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi niMwenyezi Mungu? Na hali naye amekujieni na hoja zilizowazi? Na akiwa yeye mwongo basi uwongo wake ni juuyake mwenyewe, na akiwa mkweli yatakufikieni baadhi yahayo anayo kuahidini. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoiapindukiaye mipaka, mwongo mkubwa.