[41.44] Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeniwangeli sema: Kwanini Aya zake haziku pambanuliwa?Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur'ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Nawasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwaoimezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.
[41.47] UJUZI wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tuMwenyezi Mungu. Na matunda hayatoki katika mafumbayake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayo waita,akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo watasema:Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anaye shuhudia hayo.
[41.50] Na pindi tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baadaya kumgusa dhara, bila ya shaka husema: Hayanayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja.Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu Mlezi bila yashaka nina mema yangu kwake! Basi kwa yakini tutawaelezea walio kufuru hayo waliyo yatenda,na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu.