[43.32] Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wakoMlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katikauhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yaowanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema zaMwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.