[47.4] Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingonimwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tenawaachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vitavipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Munguangeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababuakutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwakatika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao.
[47.15] Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito yamaji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribikaladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao,na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwana kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Molawao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumboyao?
[47.38] Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia yaMwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanyaubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, nanyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watuwengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.