[49.9] Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana,basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumumwenzie, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudibasi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki.Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki.
[49.12] Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwanibaadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, walamsisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.