[57.10] Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya MwenyeziMungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni waMwenyezi Mungu? Hawawi sawa miongoni mwenu wenye kutoakabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana darajakubwa zaidi kuliko wale ambao walio toa baadae nawakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.
[57.20] Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, napumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu nakushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake,kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawamabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya duniasi chochote ila ni starehe ya udanganyifu.
[57.25] Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa daliliwaziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani,ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na iliMwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wakekwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.
[57.27] Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, natukamfuatisha Isa bin Mariamu, na tukampa Injili. Natukajaalia katika nyoyo za walio mfuata upole na rehema. Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao.Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi zaMwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyo takiwa kuufuata. Basi wale walio amini katika wao tuliwapaujira wao. Na wengi wao ni wapotovu.