[58.7] Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomokatika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwimnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao,wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wawachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeyeyu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyamaatawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu niMjuzi wa kila kitu.
[58.8] Kwani huwaoni wale walio katazwa kunong'onezanakisha wakayarudia yale yale waliyo katazwa, nawakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, naya kumuasi Mtume? Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyokuamkia Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao:Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo? Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyomarejeo maovu yaliyoje!
[58.11] Enyi mlio amini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katikamabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Munguatakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: Ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua walio aminimiongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. NaMwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
[58.22] Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Sikuya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Munguna Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Haoameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwaRoho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. MwenyeziMungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndioHizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.