[61.6] Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana waIsraili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu,ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katikaTaurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kujabaada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waleteahoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi uliodhaahiri!
[61.14] Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa MwenyeziMungu, kama alivyo sema Isa bin Mariamu kuwaambiawanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa MwenyeziMungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi waMwenyezi Mungu! Basi taifa moja la Wana wa Israili liliamini, na taifa jingine lilikufuru.Basi tukawaunga mkono walio amini dhidi ya maadui zao,wakawa wenye kushinda.