[66.8] Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu tobailiyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutienimaovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilishaNabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwendambele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, nautughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kilakitu.