The Muslims Internet Directory
SURAT ANNAZIA'AT
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT ANNAZIA'AT
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[79.1] Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu,
[79.2] Na kwa wanao toa kwa upole,
[79.3] Na wanao ogelea,
[79.4] Wakishindana mbio,
[79.5] Wakidabiri mambo.
[79.6] Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
[79.7] Kifuate cha kufuatia.
[79.8] Siku hiyo nyoyo zitapiga piga,
[79.9] Macho yatainama chini.
[79.10] Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye haliya kwanza?
[79.11] Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
[79.12] Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!
[79.13] Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
[79.14] Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
[79.15] Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
[79.16] Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifula T'uwaa, akamwambia:
[79.17] Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
[79.18] Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
[79.19] Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upatekumcha.
[79.20] Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
[79.21] Lakini aliikadhibisha na akaasi.
[79.22] Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
[79.23] Akakusanya watu akanadi.
[79.24] Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
[79.25] Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwala mwisho na la mwanzo.
[79.26] Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa.
[79.27] Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu?Yeye ndiye aliye ijenga!
[79.28] Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
[79.29] Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchanawake.
[79.30] Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
[79.31] Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
[79.32] Na milima akaisimamisha,
[79.33] Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.
[79.34] Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
[79.35] Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,
[79.36] Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
[79.37] Basi ama yule aliye zidi ujeuri,
[79.38] Na akakhiari maisha ya dunia,
[79.39] Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
[79.40] Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Molawake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
[79.41] Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
[79.42] Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
[79.43] Una nini wewe hata uitaje?
[79.44] Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
[79.45] Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenyekuikhofu.
[79.46] Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa)hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN