The Muslims Internet Directory
SURAT AL-MUT'AFFIFIIN
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT AL-MUT'AFFIFIIN
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[83.1] Ole wao hao wapunjao!
[83.2] Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
[83.3] Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizanihupunguza.
[83.4] Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
[83.5] Katika Siku iliyo kuu,
[83.6] Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwenguwote?
[83.7] Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shakayamo katika Sijjin.
[83.8] Unajua nini Sijjin?
[83.9] Kitabu kilicho andikwa.
[83.10] Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
[83.11] Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
[83.12] Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka,mwenye dhambi.
[83.13] Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wakale!
[83.14] Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao haowalio kuwa wakiyachuma.
[83.15] Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shakawatazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
[83.16] Kisha wataingia Motoni!
[83.17] Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwamkiyakadhabisha.
[83.18] Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shakayamo katika I'liyyin.
[83.19] Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?
[83.20] Kitabu kilicho andikwa.
[83.21] Wanakishuhudia walio karibishwa.
[83.22] Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katikaneema.
[83.23] Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
[83.24] Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
[83.25] Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
[83.26] Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindaniewenye kushindana.
[83.27] Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
[83.28] Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
[83.29] Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwawakiwacheka walio amini.
[83.30] Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana.
[83.31] Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
[83.32] Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasawalio potea.
[83.33] Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
[83.34] Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
[83.35] Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
[83.36] Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwawakiyatenda?
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN