The Muslims Internet Directory
SURAT MARYAM
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT MARYAM
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[19.1] Kaf Ha Ya A'yn S'ad
[19.2] Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwamja wake, Zakariya.
[19.3] Alipo mwita Mola wake Mlezi kwa siri.
[19.4] Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yanguyamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala,Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwakukuomba Wewe.
[19.5] Na hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu.Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako.
[19.6] Atakaye nirithi mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub.Ewe Mola wangu Mlezi! Na umjaalie awe mwenyekuridhisha.
[19.7] (Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisitunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapatakumpa jina hilo yeyote kabla yake.
[19.8] Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa namwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimesha fikiaukongwe katika uzee?
[19.9] Akasema: Ndio hivyo hivyo amesema Mola wako Mlezi:Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwishakuumba wewe zamani na hali hukuwa kitu.
[19.10] Akasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. AkasemaIshara yako ni kuwa hutasema na watu kwa masikumatatu, na hali ni mzima.
[19.11] Basi akawatokea watu wake kutoka mihirabuni.Akawaashiria: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi najioni.
[19.12] Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpahikima angali mtoto.
[19.13] Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, naakawa mchamungu.
[19.14] Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabarimua'si.
[19.15] Na amani iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku yakufa, na siku ya kufufuliwa.
[19.16] Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitengana jamaa zake mahali upande wa mashariki;
[19.17] Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Rohowetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.
[19.18] (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwaMwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.
[19.19] (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwana Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwanaaliye takasika.
[19.20] Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyotehajanigusa, wala mimi si kahaba?
[19.21] (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wakoMlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanyekuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
[19.22] Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpakamahali pa mbali.
[19.23] Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende;akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawaniliye sahaulika kabisa!
[19.24] Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike!Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijitokidogo cha maji!
[19.25] Na litikise kwako hilo shina la mtende,utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
[19.26] Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Napindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika miminimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwahivyo leo sitasema na mtu.
[19.27] Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba.Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu!
[19.28] Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu,wala mama yako hakuwa kahaba.
[19.29] Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemezealiye bado mdogo yumo katika mlezi?
[19.30] (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa MwenyeziMungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii.
[19.31] Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote paleniwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai,
[19.32] Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanyaniwe jeuri, mwovu.
[19.33] Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na sikunitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.
[19.34] Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli yahaki ambayo wanaifanyia shaka.
[19.35] Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu,Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambiatu: Kuwa! Likawa.
[19.36] Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, naMola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo NjiaIliyo Nyooka.
[19.37] Lakini makundi yakakhitalifiana wao kwa wao. Basiole wao hao walio kufuru kwa kuhudhuria Siku iliyokuu!
[19.38] Watasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayotufikia! Lakini madhaalimu sasa wamo katika upotofuulio dhaahiri.
[19.39] Na waonye siku ya majuto itapo katwa amri. Naowamo katika ghafla, wala hawaamini.
[19.40] Hakika Sisi tutairithi ardhi na walio juu yake. Nakwetu watarejeshwa.
[19.41] Na mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeyealikuwa mkweli, Nabii.
[19.42] Alipo mwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa niniunaabudu visivyo sikia, na visivyo ona, na visivyokufaa chochote?
[19.43] Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia ilimu isiyokufikia wewe. Basi nifuate mimi, nami nitakuongozaNjia Iliyo Sawa.
[19.44] Ewe baba yangu! Usimuabudu Shet'ani. HakikaShet'ani ni mwenye kumuasi Mwingi wa Rehema.
[19.45] Ewe baba yangu! Hakika mimi naogopa isikupateadhabu inayo toka kwa Mwingi wa Rehema ukaja kuwamwenziwe Shet'ani.
[19.46] (Baba) akasema: Unaichukia miungu yangu, eweIbrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Naniondokelee mbali kwa muda!
[19.47] (Ibrahim) akasema: Salamun a'laika! Amani iwe juuyako! Mimi nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi.Hakika Yeye ananihurumia sana.
[19.48] Nami najitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badalaya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi;asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi.
[19.49] Basi alipo jitenga nao na yale waliyo kuwawakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimpa Is-haqna Yaaqub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.
[19.50] Na tukawapa rehema zetu na tukawajaalia kupewasifa za kweli tukufu.
[19.51] Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwani mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii.
[19.52] Na tulimwita upande wa kulia wa mlima natukamsogeza kunong'ona naye.
[19.53] Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, aweNabii.
[19.54] Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeyealikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.
[19.55] Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zaka, naalikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa.
[19.56] Na mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwani mkweli Nabii.
[19.57] Na tulimuinua daraja ya juu.
[19.58] Hao ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongonimwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wawale tulio wapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzaowa Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa natukawateuwa. Wanapo somewa Aya za Mwingi wa Rehemahuanguka kusujudu na kulia.
[19.59] Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaachaSala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kutamalipo ya ubaya.
[19.60] Isipo kuwa walio tubu, wakaamini, na wakatendamema. Hao, basi, wataingia Peponi wala hawatadhulumiwachochote.
[19.61] Bustani za milele alizo waahidi Rahmani waja wakekatika siri. Hakika ahadi yake hapana shaka itafika.
[19.62] Humo hawatasikia upuuzi, ila Salama tu. Nawatapata humo riziki zao asubuhi na jioni.
[19.63] Hiyo ndiyo Pepo tutayo warithisha katika waja wetuwalio kuwa wachamngu.
[19.64] (Nao watasema:) Wala hatuteremki ila kwa amri yaMola wako Mlezi. Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu nayaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.
[19.65] Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo bainayake. Basi muabudu Yeye tu, na udumu katika ibadayake. Je, mnamjua mwenye jina kama lake?
[19.66] Na mwanaadamu husema: Hivyo, nitakapo kufa, nikweli nitafufuliwa niwe hai tena?
[19.67] Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumbakabla, na hali hakuwa chochote?
[19.68] Basi naapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakinitutawakusanya wao pamoja na mashet'ani; kishatutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu, nao wamepigamagoti!
[19.69] Kisha kwa yakini tutawatoa katika kila kundi walemiongoni mwao walio zidi kumuasi Arrahmani, Mwingi waRahema..
[19.70] Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo.
[19.71] Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenyekuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayolazima itimizwe.
[19.72] Kisha tutawaokoa wale walio mchamngu; natutawaacha madhaalimu humo wamepiga magoti.
[19.73] Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, waliokufuru huwaambia walio amini: Lipi katika makundimawili lenye cheo kizuri na lilio bora barazani?
[19.74] Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizo kuwa namapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi kwa kuwatazama!
[19.75] Sema: Walio katika upotofu basi Arrahmani Mwingiwa Rahema atawapururia muda mpaka wayaone waliyo onywa- ama ni adhabu au ni Saa. Hapo ndipo watapo jua ni nani mwenye makao mabaya na mwenye askari dhaifu.
[19.76] Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wenyekushika uwongofu. Na mema yenye kudumu ni bora katikamalipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana mwisho mwema.
[19.77] Je, umemwona aliye zikanya Ishara zetu na akasema:Kwa hakika mimi nitapewa mali na wana!
[19.78] Kwani yeye amepata khabari za ghaibu, au amechukuaahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema?
[19.79] Hasha! Tutaandika anayo yasema, tutamkunjulia mudawa adhabu.
[19.80] Na tutamrithi hayo anayo yasema, na atatufikiamtupu peke yake!
[19.81] Na wamechukua miungu mingine badala ya MwenyeziMungu ili ati iwape nguvu.
[19.82] Sivyo kabisa! Wataikataa hiyo ibada yao, nawatakuwa ndio dhidi yao.
[19.83] Kwani huoni ya kwamba tumewatuma mashet'ani kwamakafiri wawachochee kwa uchochezi?
[19.84] Basi usiwafanyie haraka. Sisi tunawahisabia idadiya siku zao.
[19.85] Siku tutayo wakusanya wachamngu kuwapeleka kwaArrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni wageni wake.
[19.86] Na tukawachunga wakhalifu kuwapeleka Jahannamuhali ya kuwa wana kiu.
[19.87] Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi ila wale waliochukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema..
[19.88] Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehemaana mwana!
[19.89] Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
[19.90] Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhikupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.
[19.91] Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema anamwana.
[19.92] Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa namwana.
[19.93] Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ilaatafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwawake.
[19.94] Yeye hakika amewadhibiti na amewahisabu sawa sawa.
[19.95] Na kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Kiyamapeke yake.
[19.96] Hakika walio amini na wakatenda mema ArrahmaniMwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi.
[19.97] Na hakika tumeifanya nyepesi (Qur'ani) kwa ulimiwako, ili uwabashirie kwayo wachamngu, na uwaonyekwayo watu wabishi.
[19.98] Na kaumu ngapi tumezihiliki kabla yao. Je!Unawaona hata mmoja katika wao au unasikia hatamchakato wao? .
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN