[2.26] Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hatawa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walio aminihujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analokusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huuhuwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapoteziila wale wapotovu,

[2.61] Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumiliachakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wakoMlezi atutolee vile vinavyo mea katika ardhi, kamamboga zake, na matango yake, na thom zake, na adesizake, na vitunguu vyake. Akasema: Mnabadili kilichoduni kwa kilicho bora? Shukeni mjini, huko mtapatamlivyo viomba. Na wakapigwa na unyonge,na umasikini,na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya nikwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasipo haki. Hayo ni kwawalivyo asi na wakapindukia mipaka.

[2.74] Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hatazikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna maweyanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwasababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungusi mwenye kughafilika na mnayo yafanya.

[2.85] Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoabaadhi yenu majumbani kwao, mkisaidiana kwa dhambi nauadui. Na wakikujieni mateka mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu namnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutendahayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabukali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilikana yale mnayo yatenda.

[2.90] Kiovu kweli walicho jiuzia nafsi zao, nacho nikule kukataa kwao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, kwaajili ya kuona maya kwa kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia fadhila yake amtakaye miongoni mwa wajawake. Basi wamejiletea wenyewe ghadhabu juu yaghadhabu. Na makafiri watapata mateso ya kudhalilisha.

[2.102] Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzuliaufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, balimashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili,Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala haohawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi nimtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawiliyale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezikumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Nawanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Nahakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mnowalicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.

[2.109] Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lauwange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada yakuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani yanafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basisameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Munguatapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muwezawa kila kitu.

[2.113] Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. NaWakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo. Na ilhaliwote wanasoma Kitabu hicho hicho (Biblia). Na kadhaalika walisema wale wasio jua kitu mfano wa kauliyao hii. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Sikuya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitilafiana.

[2.125] Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (yaAlkaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala paamani. Na alipo kuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail:Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwakut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanao inama na kusujudu.

[2.136] Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yaletuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwaIbrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake,na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabiiwengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishibaina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.

[2.140] Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak naYaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo?Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? NaMwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo.

[2.143] Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wawasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume aweni shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulichokuwa nacho ila tupate kumjua yule anaye mfuata Mtumena yule anaye geuka akarejea nyuma. Na kwa yakini hilolilikuwa jambo gumu isipo kuwa kwa wale alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenyekuipoteza Imani yenu. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mpolekwa watu na Mwenye kuwarehemu.

[2.144] Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wakombinguni. Basi tutakuelekeza kwenye Kibla ukipendacho.Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo; nahakika wale walio pewa Kitabu wanajua kwamba hiyo nihaki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda.

[2.164] Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, nakukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazohupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayoakaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humokila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu naardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.

[2.165] Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpendaMwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda MwenyeziMungu zaidi sana. Na laiti walio dhulumu wakajuawatakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za MwenyeziMungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu!

[2.177] Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wamashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muaminiMwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaana mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, nakatika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; haondio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.

[2.178]Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasikatika walio uwawa - muungwana kwa muungwana, namtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipakwa wema, na yeye alipe kwa ihsani. Huko nikupunguziwa kuliko tokana na Mola wenu Mlezi, na nirehema. Na atakaye vuka mipaka baada ya haya, basiyeye atapata adhabu chungu.

[2.185] Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humoQur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo waziza uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa ausafarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine.Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, namumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ilimpate kushukuru.

[2.187] Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wakezenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao.Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu naamekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takenialiyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katikaweusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Walamsichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basimsiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainishaIshara zake kwa watu ili wapate kumcha.

[2.196] Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya MwenyeziMungu. Na ikiwa mkizuiwa,basi (chinjeni) wanyama waliowepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Naatakaye kuwa mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwanimwake basi atoe fidiya kwa kufunga au kwa kutoa sadakaau kuchinja wanyama. Na mtakapo kuwa salama, basimwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndioakahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Naasiye pata, afunge siku tatu katika Hija na siku sabamtakapo rudi; hizi ni kumi kaamili. Hayo ni kwa ajiliya yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni MwenyeziMungu ni Mkali wa kuadhibu.

[2.197] Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanyaHija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafuwala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Munguanaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora yazawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!

[2.213] Watu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Munguakapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja naoakateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na walahawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hichobaada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhiniyake akawaongoa walio amini kwendea haki katika mambowaliyo khitalifiana. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka.

[2.217] Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezimtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambikubwa. Lakini kuzuilia watu wasende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watuwasende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wakehumo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala hawatoachakupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kamawakiweza. Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao a'malizao zimeharibika duniani na Akhera. Na hao ndio watuwa Motoni; humo watadumu.

[2.220]--katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera. Nawanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndiokheri. Na mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu; na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. NaMwenyezi Mungu angeli penda angeli kutieni katikaudhia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenyehikima.

[2.221] Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini.Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hataakikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muuminini bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Haowanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaitia kwenyePepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainishaAya zake kwa watu ili wapate kukumbuka.

[2.228] Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpakat'ahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuziikuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao,ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Nawaume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo,kama wakitaka kufanya sulhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Nawanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na MwenyeziMungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

[2.229]T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema aukuachana kwa vizuri. Wala si halali kwenu kuchukuachochote mlicho wapa wake zenu, ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipakaya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawatawezakushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapana lawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyomipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na watakaoikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhaalimu.

[2.231] Na mtakapo wapa wanawake t'alaka, nao wakafikiakumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema auwaachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye fanya hivyo, amejidhulumunafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungukwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabuna hikima anacho kuonyeni kwacho. Na mcheni MwenyeziMungu, na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

[2.232] Na mtakapo wapa wanawake t'alaka nao wakamalizaeda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapobaina yao wamepatana kwa wema. Hayo anaonywa nayo yule miongoni mwenu anaye muamini Mwenyezi Mungu naSiku ya Mwisho. Hayo ni bora zaidi kwenu na safikabisa. Na Mwenyezi Mungu anajua, lakini nyinyihamjui.

[2.233] Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miakamiwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Najuu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwakadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajiliya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitakakumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basisi vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoamlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni MwenyeziMungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.

[2.235] Wala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwaishara tu kwa wanawake waliomo edani au mkadhamiriakatika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, ilamnene maneno mema. Wala msiazimie kufunga ndoa mpakaeda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo katika nafsi zenu. Basitahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu niMwenye kusamehe na Mpole.

[2.237] Na mkiwapa t'alaka kabla ya kuwagusa, nammekwisha wawekea hayo mahari makhsusi, basi wapeninusu ya mahari mlio agana, isipo kuwa ikiwa wanawake wenyewe wamesamehe, au mume ambaye kifungo cha ndoa kimikononi mwake awe amesamehe. Na kusameheana ndikokulio karibu zaidi na uchamngu. Wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaonamnayo yatenda.

[2.240] Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawachawake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizikwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumba. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu kwa waliyojifanyia wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na MwenyeziMungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

[2.246] Hukuwaona watukufu katika Wana wa Israili baadaya Musa, walipo mwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ilitupigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Je, haielekei ikiwa mtaandikiwa vita kuwa msipigane?Wakasema: Itakuwaje tusipigane katika Njia ya MwenyeziMungu, na hali tumetolewa majumbani kwetu na watoto wetu? Lakini walipo andikiwa kupiganawaligeuka, isipo kuwa wachache miongoni mwao. NaMwenyezi Mungu anawajua madhaalimu.

[2.247], Na Nabii wao akawaambia: Mwenyezi Munguamekuteulieni Taluti (Sauli) kuwa ni mfalme. Wakasema:vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tunahaki zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewawasaa wa mali? Akasema: Mwenyezi Mungu amemteua yeyejuu yenu na amemzidishia ukunjufu wa ilimu nakiwiliwili. Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wakeamtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mjuzi.

[2.249] Basi Taluti alipo ondoka na majeshi alisema:Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywahumo si pamoja nami, na asiye kunywa atakuwa pamoja nami: ila atakaye teka kiasi ya kitanga cha mkonowake. Lakini walikunywa humo isipo kuwa wachache tumiongoni mwao. Alipo vuka mto yeye na wale walio aminipamoja naye, walisema: Leo hatumwezi Jaluti (Goliati)na majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini yakukutana na Mwenyezi Mungu: Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya MwenyeziMungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.

[2.251]--Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu waliwatimua, naDaudi akamuuwa Jaluti, na Mwenyezi Mungu akampa Daudiufalme na hikima, na akamfundisha aliyo yapenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watubasi dunia ingeli haribika. Lakini Mwenyezi Mungu niMwenye fadhila juu ya walimwengu wote.

[2.253] MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu yawengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisemanao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isamwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvukwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipendawasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajiahoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapokati yao walio amini, na wengine kati yao waliokufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.

[2.255] Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai,Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi walakulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yakebila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao nayaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe.Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na walahaemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu,na ndiye Mkuu.

[2.258] Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu yaMola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpaufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuishana kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Munguhulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na MwenyeziMungu hawaongoi watu madhaalimu.

[2.259] Au kama yule aliye pita karibu na mji ulio kwishakuwa magofu tu, akasema: Ataufufuaje Mwenyezi Mungumji huu baada ya kufa kwake? Basi Mwenyezi Mungu alimfisha yeye muda wa miaka mia. Kisha akamfufua.Akamuuliza: Je umekaa muda gani? Akajibu: Labdanimekaa siku moja au sehemu ya siku. Akamwambia: Bali umekaa miaka mia wewe. Hebu angalia chakula chako navinywaji vyako, havikuharibika. Na muangalie pundawako. Na ili tukufanye uwe ni Ishara kwa watu iangalie hii mifupa yake jinsi tunavyo inyanyua kishatunaivisha nyama. Basi yalipo mbainikia alinena: Najuakwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

[2.260] Na alipo sema Ibrahim: Mola wangu Mlezi!Nionyeshe vipi unavyo fufua wafu. Mwenyezi Munguakasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ilimoyo wangu utue. Akamwambia: Twaa ndege wane nauwazoeshe kwako, kisha uweke juu ya kila kilima sehemu, kisha wete, watakujia mbio. Na ujuekwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu,na Mwenye hikima.

[2.264] Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwamasimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwakuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wajabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa namvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoiwatu makafiri.

[2.265] Na mfano wa wale wanao toa mali zao kwa kuitafutaradhi ya Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao nikama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mardufu; na hata kamahaifikiwi na mvua kubwa basi manyunyu hutosha. NaMwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.

[2.266] Je! Yupo mmoja wenu anaye penda kuwa na kitalucha mitende na mizabibu ipitayo mito kati yake, nayehumo hupata mazao ya kila namna, na uzee ukamfikia naye hali ana watoto wanyonge, kikapigwa na kimbungachenye moto, kikaungua? Hivi ndivyo Mwenyezi Munguanavyo kubainishieni Ishara ili mpate kufikiri.

[2.273] Nawapewe mafakiri walio zuilika katika njia zaMwenyezi Mungu, wasio weza kusafiri katika nchikutafuta riziki. Asiye wajua hali zao huwadhania kuwani matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambuakwa alama zao; hawang'ang'analii watu kwa kuwaomba. Nakheri yoyote mnayo toa, basi kwa yakini Mwenyezi Mungu anaijua.

[2.275] Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simamaaliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwawamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wakeMlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenyekurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.

[2.282] Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa mudaulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike bainayenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenyedeni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu,Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyongeau hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinziwake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaumewawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katikamnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidiwasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika denilikiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwaushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwani biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapouziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatanimwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo basi hakikahilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. NaMwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

[2.283] Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatoshakukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amanamwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi.Wala msifiche ushahidi. Na atakaye ficha basi hakikamoyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mnayo yatenda.

[2.285] Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwaMola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wotewamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabuvyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyotekatika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia natumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.

[2.286] Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwakadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake,na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau autukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kamaulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, nautughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu.Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri.
