[20.40] Dada yako alipo kwenda na akasema: Je!Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? Basitukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike,wala asihuzunike. Na ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoakatika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kamailivyo kadiriwa, ewe Musa!
[20.71] (Firauni) akasema: Oh! Mnamuamini kabla sijakupeniruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliyekufundisheni uchawi. Basi kwa yakini nitakukatenimikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Nanitakutundikeni misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisialiye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake.