The Muslims Internet Directory
SURATUL ANBIYAA
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURATUL ANBIYAA
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[21.1] IMEWAKARIBIA watu hisabu yao, nao wamo katikamghafala wanapuuza.
[21.2] Hayawafikilii mawaidha mapya kutoka kwa Mola waoMlezi ila huyasikiliza na huku wanafanya mchezo.
[21.3] Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumuhunong'onezana kwa siri: Ni nani ati huyu isipo kuwani binaadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea uchawi hali nanyi mnaona?
[21.4] Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayombinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikiaMwenye kujua.
[21.5] Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo,bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basiatuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo.
[21.6] Hawakuamini kabla yao watu wa mji tulio uangamiza.Basi, je, wataamini hawa?
[21.7] Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tuliowapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ilimu ikiwanyinyi hamjui.
[21.8] Wala hatukuwafanya miili isiyo kula chakula, walahawakuwa wenye kuishi milele.
[21.9] Kisha tukawatimizia miadi, na tukawaokoa wao natulio wataka, na tukawateketeza walio pita mipaka.
[21.10] Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndaniyake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?
[21.11] Na mingapi katika miji iliyo kuwa ikidhulumutumeiteketeza, na tukawasimamisha baada yao watuwengine.
[21.12] Basi walipo ihisi adhabu yetu, mara wakaanzakukimbia.
[21.13] Msikimbie! Na rejeeni kwenye zile zile starehezenu, na maskani zenu, mpate kusailiwa!
[21.14] Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwamadhaalimu.
[21.15] Hakikuacha hicho kuwa kilio chao mpaka tukawafanyakama walio fyekwa, wamezimika.
[21.16] Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo bainayao kwa mchezo.
[21.17] Kama tungeli taka kufanya mchezo tunge jifanyiaSisi wenyewe, lau kwamba tungeli kuwa ni wafanyaomchezo.
[21.18] Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja namara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua.
[21.19] Na ni vyake Yeye tu Mwenyezi Mungu vilivyomombinguni na katika ardhi. Na walioko kwake hawafanyikiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki.
[21.20] Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei.
[21.21] Au wamepata miungu katika ardhi inayo fufua?
[21.22] Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwaMwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhizingeli fisidika. Subahana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi), nahayo wanayo yazua.
[21.23] Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaohojiwa kwa wayatendayo.
[21.24] Au wanawaabudu miungu mingine badala yake? Sema:Leteni ushahidi wenu! Haya ni ukumbusho wa hawa walionami, na ukumbusho wa walio kabla yangu. Lakini wengi wao hawaijui kweli, na kwa hivyo wanapuuza.
[21.25] Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ilatulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi.Basi niabuduni Mimi tu.
[21.26] Na wanasema: Arrahman, Mwingi wa Rehema, anamwana! Subhanahu, Ametakasika na hayo! Bali hao (wanaowaita wana) ni watumwa walio tukuzwa.
[21.27] Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake.
[21.28] Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao.Wala hawamwombei yeyote ila yule anaye mridhia Yeye,nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea.
[21.29] Na yeyote kati yao atakaye sema: Mimi ni mungu,badala yake, basi huyo tutamlipa malipo yakeJahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wenye kudhulumu.
[21.30] Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu naardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisitukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilichohai? Basi je, hawaamini?
[21.31] Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti iliisiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapatekuongoka.
[21.32] Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa,lakini wanazipuuza Ishara zake.
[21.33] Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua namwezi, vyote katika anga vinaogelea.
[21.34] Nasi hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yakokuwa na maisha ya milele. Basi je! Ukifa wewe, waowataishi milele?
[21.35] Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwamtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.
[21.36] Na wakikuona walio kufuru hawakufanyi wewe ila nikitu cha maskhara tu, (wakisema): Je! Ndiye huyu anayeitaja miungu yenu? Na hali wao wanakataa kumkumbuka Arrahman, Mwingi wa Rehema!
[21.37] Mwanaadamu ameumbwa na haraka. NitakuonyesheniIshara zangu. Basi msinihimize.
[21.38] Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyimnasema kweli?
[21.39] Lau wangeli jua wale walio kufuru wakati ambaohawatauzuia Moto kwenye nyuso zao wala migongo yao, nawala hawatanusuriwa!
[21.40] Bali utawafikia kwa ghafla, na utawashitua na walahawataweza kuurudisha, wala hawatapewa muhula!
[21.41] Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa.Kwa hivyo wale walio wafanyia maskhara yaliwafika yalewaliyo kuwa wakiyafanyia dhihaka.
[21.42] Sema: Nani anaye kulindeni usiku na mchana naArrahmani Mwingi wa Rehema? Bali wao wanapuuzakumkumbuka Mola wao Mlezi.
[21.43] Au wao wanao miungu watao weza kuwakinga nasi? Haohawawezi kujinusuru nafsi zao, wala hawatalindwa nasi!
[21.44] Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umriukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisitunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Haoni wenye kushinda?
[21.45] Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi. Na viziwihawasikii wito wanapo onywa.
[21.46] Na wanapo guswa na mpulizo mmoja tu wa adhabuitokayo kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka wao husema:Ole wetu! Hakika tulikuwa wenye kudhulumu.
[21.47] Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku yaKiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hataikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasitunatosha kuwa washika hisabu.
[21.48] Na kwa yakini tuliwapa Musa na Haarunikipambanuzi, na mwangaza, na makumbusho kwa wachamngu,
[21.49] Ambao wanamkhofu Mola wao Mlezi faraghani, nawanaiogopa Saa ya Kiyama.
[21.50] Na haya ni makumbusho yaliyo barikiwa, tuliyoyateremsha. Basi je! Mnayakataa?
[21.51] Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu wakezamani, na tulikuwa tunamjua.
[21.52] Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini hayamasanamu mnayo yashughulikia kuyaabudu?
[21.53] Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.
[21.54] Akasema: Bila ya shaka nyinyi na baba zenu mmekuwakatika upotofu ulio dhaahiri.
[21.55] Wakasema: Je! Umetujia kwa maneno ya kweli au weweni katika wachezao tu?
[21.56] Akasema: Bali Mola wenu Mlezi ni Mola Mlezi wambingu na ardhi ambaye ndiye aliye ziumba. Na mimi nikatika wenye kuyashuhudia hayo.
[21.57] Na Wallahi! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenuhaya baada ya mkisha geuka kwenda zenu.
[21.58] Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao,ili wao walirudie.
[21.59] Wakasema: Nani aliye ifanyia haya miungu yetu?Hakika huyu ni katika walio dhulumu.
[21.60] Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja.Anaitwa Ibrahim.
[21.61] Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu, wapatekumshuhudia!
[21.62] Wakasema: Je! Wewe umeifanyia haya miungu yetu,ewe Ibrahim?
[21.63] Akasema: Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao. Basiwaulizeni ikiwa wanaweza kutamka.
[21.64] Basi wakajirudi nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyimlikuwa madhaalimu!
[21.65] Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu waowakasema: Wewe unajua kwamba hawa hawesemi.
[21.66] Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwaMwenyezi Mungu wasio kufaini kitu wala kukudhuruni?
[21.67] Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyo viabudu badala yaMwenyezi Mungu! Basi nyinyi hamtii akilini?
[21.68] Wakasema: Mchomeni moto, na muinusuru miungu yenu,ikiwa nyinyi ni watendao jambo!
[21.69] Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwaIbrahim!
[21.70] Wao walimkusudia maovu, lakini Sisi tukawafanyawao ndio walio khasiri.
[21.71] Na tukamwokoa yeye na Luut'i tukawapeleka kwenyenchi tulio ibariki kwa ajili ya walimwengu wote.
[21.72] Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Nawote tukawajaalia wawe watu wema.
[21.73] Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amriyetu. Na tukawafunulia watende kheri, na washike Sala,na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu.
[21.74] Na Luut'i tukampa hukumu na ilimu na tukamwokoa naule mji ulio kuwa ukifanya maovu. Hakika hao walikuwawatu wabaya, wachafu.
[21.75] Na tukamuingiza katika rehema yetu. Hakika yeye nimiongoni mwa watenda mema.
[21.76] Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, natukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa.
[21.77] Na tukamnusuru na watu walio zikanusha Isharazetu. Hakika hao walikuwa watu wabaya. Basitukawazamisha wote.
[21.78] Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katikakadhiya ya konde walipo lisha humo mbuzi wa watuusiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yaohiyo.
[21.79] Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpahukumu na ilimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwapamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo.
[21.80] Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajiliyenu ili yakuhifadhini katika kupigana kwenu. Je!Mtakuwa wenye kushukuru?
[21.81] Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbungawendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyo ibarikia. NaSisi ndio tunao jua kila kitu.
[21.82] Na pia mashet'ani wanao mpigia mbizi na kufanyakazi nyenginezo. Na Sisi tulikuwa walinzi wao.
[21.83] Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema:Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemukuliko wote wanao rehemu.
[21.84] Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamojanao kuwa ni rehema inayo toka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada.
[21.85] Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli - wote walikuwamiongoni mwa wanao subiri.
[21.86] Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika waowalikuwa katika watu wema.
[21.87] Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, naakadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basialiita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwamiongoni mwa wenye kudhulumu.
[21.88] Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki.Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini.
[21.89] Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Molawangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mborawa wanao rithi.
[21.90] Basi tukamwitikia, na tukampa Yahya natukamponyeshea mkewe. Hakika wao walikuwa wepesi wakutenda mema, na wakituomba kwa shauku na khofu. Naowalikuwa wakitunyenyekea.
[21.91] Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampuliziakatika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwani Ishara kwa walimwengu.
[21.92] Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi niMola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.
[21.93] Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapandebaina yao. Wote watarudi kwetu.
[21.94] Na atendaye mema naye ni Muumini basihaitakataliwa juhudi yake. Na hakika Sisitunamwandikia.
[21.95]Na haiwi kwa wana-mji tulio uangamiza, ya kwambahawatarejea,
[21.96] Mpaka watapo funguliwa Juju na Maajuju wakawawanateremka kutoka kila mlima;
[21.97] Na miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatapokodoka macho ya walio kufuru (na watasema:) Ole wetu!Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu.
[21.98] Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala yaMwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu.
[21.99] Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wotewatadumu humo.
[21.100] Lao wao humo ni kupiga mayowe, na walahawatasikia (jenginelo).
[21.101] Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, haowatatenganishwa na hayo.
[21.102] Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katikayale zinayo yatamani nafsi zao.
[21.103] Hicho Kitisho Kikubwa hakito wahuzunisha. NaMalaika watawapokea (kwa kuwaambia): Hii ndiyo Sikuyenu mliyo kuwa mkiahidiwa!
[21.104] Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wakaratasi za vitabu. Kama tulivyo anza umbo la mwanzotutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao.
[21.105] Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baadaya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wanguwalio wema.
[21.106] Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watuwafanyao ibada.
[21.107] Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwawalimwengu wote.
[21.108] Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakikaMungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?
[21.109] Na kama wakigeuka, basi sema: Nimekutangazienisawa sawa, wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyoahidiwa.
[21.110] Hakika Yeye anajua kauli ya dhaahiri na anajuamyafichayo.
[21.111] Wala sijui pengine huu ni mtihani tu kwenu nastarehe mpaka muda kidogo.
[21.112] Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Molawetu Mlezi ni Mwingi wa Rehema, aombwaye msaada juu yamnayo yazua.
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN