The Muslims Internet Directory
SURAT ASH-SHUA'RAA
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Library ↓
Prayer Times
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Classifieds ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
More... ↓
Login/Register
Muslims Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Islamic Classifieds
WebRing Sites
Help/FAQ
Help?
-
Live!
Advertisement
:
Featured Site
Feature Your Site Now
Paid Services
Buy The Islamic CD
Banner Design
Submit Your Site
Muslims Million Pixels
2Muslims Services
Free E-mail Account
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
New
Free Guestbook
New
Islamic Internet Gadgets
Prayer Times Software
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Polls and Votting
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Holidays Dates
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
How To Pray?
Translate Site To:
Arabic
Bulgarian
Catalan
Chinese (Simplified)
Chinese (Traditional)
Croatian
Czech
Danish
Dutch
English
Filipino
Finnish
French
German
Greek
Hebrew
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latvian
Lithuanian
Norwegian
Polish
Portuguese
Romanian
Russian
Serbian
Slovak
Slovenian
Spanish
Swedish
Ukrainian
Vietnamese
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
view results
view other polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: SURAT ASH-SHUA'RAA
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Chinese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[26.1] T'aa Siin Miim. (T'.S.M.)
[26.2] Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
[26.3] Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawiWaumini.
[26.4] Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguniIshara zikanyenyekea shingo zao.
[26.5] Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahmanila wao hujitenga nao.
[26.6] Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikiakhabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha.
[26.7] Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeioteshahumo, ya kila namna nzuri?
[26.8] Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi waohawakuwa wenye kuamini.
[26.9] Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvuMwenye kurehemu.
[26.10] Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia:Fika kwa watu madhaalimu,
[26.11] Watu wa Firauni. Hawaogopi?
[26.12] Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe.
[26.13] Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wanguhaukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun.
[26.14] Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopawasije kuniuwa.
[26.15] Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujizayetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza.
[26.16] Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi niMitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
[26.17] Waachilie Wana wa Israili wende nasi.
[26.18] (Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni,na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi?
[26.19] Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawamiongoni mwa wasio na shukrani?
[26.20] (Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwamiongoni mwa wale walio potea.
[26.21] Basi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Molawangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwemiongoni mwa Mitume.
[26.22] Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na weweumewatia utumwani Wana wa Israili?
[26.23] Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wawalimwengu wote?
[26.24] Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, naviliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini.
[26.25] (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi?
[26.26] (Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na MolaMlezi wa baba zenu wa kwanza.
[26.27] (Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliyetumwa kwenu ni mwendawazimu.
[26.28] (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki naMagharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatiaakilini.
[26.29] (Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiyekuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani.
[26.30] Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu chakubainisha wazi?
[26.31] Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemaokweli.
[26.32] Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wakuonekana dhaahiri.
[26.33] Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwawatazamao.
[26.34] (Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka:Hakika huyu ni mchawi mtaalamu.
[26.35] Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawiwake. Basi mna shauri gani?
[26.36] Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatumemijini wapigao mbiu ya mgambo.
[26.37] Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu.
[26.38] Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu.
[26.39] Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika?
[26.40] Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakaoshinda.
[26.41] Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je!Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda?
[26.42] Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele.
[26.43] Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa.
[26.44] Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema:Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenyekushinda.
[26.45] Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimezawalivyo vizua.
[26.46] Hapo wachawi walipinduka wakasujudu.
[26.47] Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwenguwote.
[26.48] Mola Mlezi wa Musa na Harun.
[26.49] (Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kablasijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwawenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua!Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha.Na nitakubandikeni misalabani nyote.
[26.50] Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejeakwa Mola wetu Mlezi.
[26.51] Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehemakosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini.
[26.52] Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na wajawangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa.
[26.53] Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu zamgambo.
[26.54] (Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo.
[26.55] Nao wanatuudhi.
[26.56] Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari.
[26.57] Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem,
[26.58] Na makhazina, na vyeo vya hishima,
[26.59] Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana waIsraili.
[26.60] Basi wakawafuata lilipo chomoza jua.
[26.61] Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musawakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana!
[26.62] (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Molawangu Mlezi. Yeye ataniongoa!
[26.63] Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwafimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kamamlima mkubwa.
[26.64] Na tukawajongeza hapo wale wengine.
[26.65] Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote.
[26.66] Kisha tukawazamisha hao wengine.
[26.67] Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara;lakini wengi wao si katika wenye kuamini.
[26.68] Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvuMwenye kurehemu.
[26.69] Na wasomee khabari za Ibrahim.
[26.70] Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudunini?
[26.71] Wakasema: Tunaabudu masanamu, daimatunayanyenyekea.
[26.72] Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita?
[26.73] Au yanakufaeni, au yanakudhuruni?
[26.74] Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanyahivyo hivyo.
[26.75] Je! Mmewaona hawa mnao waabudu-
[26.76] Nyinyi na baba zenu wa zamani?
[26.77] Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa MolaMlezi wa walimwengu wote.
[26.78] Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiyeananiongoa,
[26.79] Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha.
[26.80] Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.
[26.81] Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha.
[26.82] Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosayangu Siku ya Malipo.
[26.83], Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishena watendao mema.
[26.84] Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kujabaadaye.
[26.85] Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema.
[26.86] Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwamiongoni mwa wapotovu.
[26.87] Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa.
[26.88] Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.
[26.89] Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyosafi.
[26.90] Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu.
[26.91] Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu.
[26.92] Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu
[26.93] Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, auwanajisaidia wenyewe?
[26.94] Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu,
[26.95] Na majeshi ya Ibilisi yote.
[26.96] Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo:
[26.97] Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu uliodhaahiri,
[26.98] Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wawalimwengu wote.
[26.99] Na hawakutupoteza ila wale wakosefu.
[26.100] Basi hatuna waombezi.
[26.101] Wala rafiki wa dhati.
[26.102] Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwakatika Waumini.
[26.103] Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi waohawakuwa wenye kuamini.
[26.104] Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvuMwenye kurehemu.
[26.105] Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume.
[26.106] Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?
[26.107] Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
[26.108] Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
[26.109] Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wanguhauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
[26.110] Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
[26.111] Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuatani watu wa chini?
[26.112] Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
[26.113] Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laitimngeli tambua!
[26.114] Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
[26.115] Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahirishaahiri.
[26.116] Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shakautapigwa mawe.
[26.117] Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wanguwamenikanusha.
[26.118] Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako,na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini.
[26.119] Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamojanaye katika marikebu iliyo sheheni.
[26.120] Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia.
[26.121] Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengiwao walio kuwa Waumini.
[26.122] Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvuMwenye kurehemu.
[26.123] Kina A'd waliwakanusha Mitume.
[26.124] Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu?
[26.125] Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
[26.126] Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
[26.127] Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wanguhauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
[26.128] Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho lakufanyia upuuzi?
[26.129] Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwambamtaishi milele!
[26.130] Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
[26.131] Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
[26.132] Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua.
[26.133] Amekupeni wanyama wa kufuga na wana.
[26.134] Na mabustani na chemchem.
[26.135] Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
[26.136] Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha auhukuwa miongoni mwa watoao mawaidha.
[26.137] Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokeazamani.
[26.138] Wala sisi hatutaadhibiwa.
[26.139] Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila yashaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengiwao wenye kuamini.
[26.140] Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvuMwenye kurehemu.
[26.141] Kina Thamud waliwakanusha Mitume.
[26.142] Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu?
[26.143] Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
[26.144] Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
[26.145] Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu haukoila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
[26.146] Je! Mtaachwa salama usalimina katika hayayaliyopo hapa?
[26.147] Katika mabustani, na chemchem?
[26.148] Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva.
[26.149] Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi.
[26.150] Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
[26.151], Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka,
[26.152] Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, walahawatengenezi.
[26.153] Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.
[26.154] Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi leteIshara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
[26.155] Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake yakunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katikasiku maalumu.
[26.156] Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeniadhabu ya Siku Kubwa.
[26.157] Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta.
[26.158] Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipoIshara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
[26.159] Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvuMwenye kurehemu.
[26.160] Watu wa Lut'i waliwakanusha Mitume.
[26.161] Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu?
[26.162] Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.
[26.163] Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.
[26.164] Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wanguhauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
[26.165] Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?
[26.166] Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezikatika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao rukamipaka!
[26.167] Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shakautakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!
[26.168] Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukiahichi kitendo chenu.
[26.169] Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu nahaya wayatendayo.
[26.170] Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,
[26.171] Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.
[26.172] Kisha tukawaangamiza wale wengine.
[26.173] Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua yawaliyo onywa.
[26.174] Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengiwao wenye kuamini.
[26.175] Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiyeMwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
[26.176] Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume.
[26.177] Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?
[26.178] Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
[26.179] Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
[26.180] Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu haukoila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
[26.181] Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katikawanao punja.
[26.182] Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;
[26.183] Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanyejeuri kwa ufisadi.
[26.184] Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyotangulia.
[26.185] Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa.
[26.186] Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, nakwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo.
[26.187] Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwawewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
[26.188] Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayoyatenda.
[26.189] Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya sikuya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa.
[26.190] Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwawengi wao wenye kuamini.
[26.191] Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiyeYeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
[26.192] Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mleziwa walimwengu wote.
[26.193] Ameuteremsha Roho muaminifu,
[26.194] Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,
[26.195] Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.
[26.196] Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabuvya kale.
[26.197] Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua hayawanazuoni wa Wana wa Israili?
[26.198] Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wawasio kuwa Waarabu,
[26.199] Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
[26.200] Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu.
[26.201] Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu.
[26.202] Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawanakhabari.
[26.203] Na watasema: Je, tutapewa muhula?
[26.204] Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?
[26.205] Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka,
[26.206] Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,
[26.207] Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
[26.208] Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa nawaonyaji -
[26.209] Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenyekudhulumu.
[26.210] Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo,
[26.211] Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.
[26.212] Hakika hao wametengwa na kusikia.
[26.213] Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na MwenyeziMungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa.
[26.214] Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
[26.215] Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwaWaumini.
[26.216] Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitengambali na hayo mnayo yatenda.
[26.217] Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenyekurehemu.
[26.218] Ambaye anakuona unapo simama,
[26.219] Na mageuko yako kati ya wanao sujudu.
[26.220] Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
[26.221] Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani?
[26.222] Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.
[26.223] Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi waoni waongo.
[26.224] Na watungaji mashairi ni wapotofu ndiowanawafuata.
[26.225] Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kilabonde?
[26.226] Na kwamba wao husema wasiyo yatenda?
[26.227] Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema,na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, nawakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumuwatakuja jua mgeuko gani watakao geuka.
Featured Ad
About Us
Contact Us
Advertise
Donate/Support
Sign Guestbook
Link To Us
Newsletter
Recommend
What's New
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Pharmacy Site
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2009
Islamic Education & Services Institute