[27.40] Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuleteakabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kionakimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru aunitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika,anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru,kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu.
[27.44] Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipoliona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpakakwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo nibehewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia):Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, nasasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.