[3.7]Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndaniyake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizomsingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano.Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zileza mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake;na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu.Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema:Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi.Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.
[3.13] Hakika ilikuwa ni Ishara kwenu katika yale majeshimawili yalipo pambana. Jeshi moja likipigana katikaNjia ya Mwenyezi Mungu, na jingine kafiri likiwaona zaidi kuliko wao mara mbili, kwa kuona kwa macho. NaMwenyezi Mungu humuunga mkono amtakaye kwa nusurayake. Hakika katika hayo yapo mazingatio kwa wenye macho.
[3.20] Na pindi wakikuhoji, basi sema: Miminimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, nakadhaalika walio nifuata. Na waambie walio pewa Kitabuna wasio na kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu basiwameongoka. Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikishaujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona wajawake.
[3.37] Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema naakamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mleziwake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu!Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwaMwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.
[3.49] Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Miminimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, yakwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege.Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya MwenyeziMungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa nawakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya MwenyeziMungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho wekaakiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.
[3.64] Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye nenolilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabuduyeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa WaolaWalezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basisemeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu.
[3.75] Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpaamana ya mrundi wa mali atakurudishia, na miongonimwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya nikwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawawasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu,hali nao wanajua.
[3.81] Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwaManabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kishaakakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juuyenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri nammekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema:Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi nipamoja nanyi katika kushuhudia.
[3.103] Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyotepamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema yaMwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyikwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwaneema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimola Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.
[3.112] Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana,isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kambaya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, nawamepigwa na unyonge. Hayo ni kwa sababu walikuwawakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakiwauwaManabii pasina haki; hayo ni kwa sababu waliasi nawalikuwa wakiruka mipaka.
[3.152] Na Mwenyezi Mungu alikutimilizieni miadi yake,vile mlivyo kuwa mnawauwa kwa idhini yake, mpaka mlipolegea na mkazozana juu ya amri, na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni mliyo yapenda. Wapo miongoni mwenuwanao taka dunia, na wapo miongoni mwenu wanao takaAkhera. Kisha akakutengeni nao (maadui) ili akujaribuni. Naye sasa amekwisha kusameheni. NaMwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini.
[3.154] Kisha baada ya dhiki alikuteremshieni utulivu -usingizi ambao ulifunika kundi moja kati yenu. Nakundi jengine nafsi zao ziliwashughulisha hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyo kuwa ya haki,dhana ya kijinga. Wakisema: Hivyo tuna lolote sisikatika jambo hili? Sema: Mambo yote ni ya MwenyeziMungu. Wanaficha katika nafsi zao wasiyo kubainishia.Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hilitusinge uliwa hapa. Sema: Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli toka walio andikiwa kufa, wakendamahali pao pa kuangukia wafe.(Haya ni hivyo) iliMwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Munguanayajua yaliyomo vifuani.
[3.156] Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio kufuru nawakawasema ndugu zao walipo safiri katika nchi auwalipo kuwa vitani: Wangeli kuwa kwetu wasingeli kufa na wasingeli uwawa. Ili Mwenyezi Mungu afanyehayo kuwa ni majuto katika nyoyo zao. Na MwenyeziMungu huhuisha na hufisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenyekuyaona myatendayo.
[3.159] Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa MwenyeziMungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwamkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, nashauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basimtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Munguhuwapenda wanao mtegemea.
[3.167] Na ili awapambanue walio kuwa wanaafiki,wakaambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya MwenyeziMungu au lindeni. Wakasema: Tungeli jua kuna kupiganabila ya shaka tungeli kufuateni. Wao siku ile walikuwakaribu na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomoyao yasiyo kuwamo nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Munguanajua kabisa wanayo yaficha.
[3.179] Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha Waumini katikahali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema. Walahaiwi kwa Mwenyezi Mungu kukujuulisheni mambo ya ghaibu. Lakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitumewake amtakaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitumeyake. Na mkiamini na mkamchamngu mtakuwa na ujira mkubwa.
[3.180] Wala wasidhani wale ambao wanafanya ubakhilikatika aliyo wapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zakekuwa ni kheri yao. Bali hiyo ni shari kwao. Watafungwakongwa za yale waliyo yafanyia ubakhili Siku yaKiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa MwenyeziMungu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yotemyatendayo.
[3.195] Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu:Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu,akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi. Basi walio hama, na walio tolewa makwao, nawakateswa katika Njia yangu, na wakapigana, nawakauliwa, kwa yakini Mimi nitawafutia makosa yao, nakwa yakini nitawaingiza katika Mabustani yanayo pitamito kati yake. Hayo ndiyo malipo yanayo toka kwaMwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu kwake yapo malipomema kabisa.