[30.9] Je! Hawatembei katika ardhi wakaona ulivyo kuwamwisho wa walio kuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvuzaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyo istawisha wao. NaMitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basihakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.