[33.4] Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyombili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu- ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanyawatoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayoni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye sema kweli, naye ndiye anaye ongoa Njia.
[33.5] Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidimbele ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa hamwajui baba zao,basi ni ndugu zenu katika Dini, na rafiki zenu. Wala si lawama juu yenu kwa mlivyo kosea. Lakini ipo lawamakatika yale ziliyo fanya nyoyo zenu kwa makusudi. NaMwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[33.19] Wana choyo juu yenu. Ikifika khofu utawaonawanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yuleambaye aliye zimia kwa kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanakuudhini kwa ndimi kali, nao nimabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini, basiMwenyezi Mungu amevibat'ilisha vitendo vyao. Na hayokwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
[33.35] Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, naWaumini wanaume na Waumini wanawake, na wat'iifuwanaume na wat'iifu wanawake, na wasemao kweli wanaumena wanawake, na wanao subiri wanaume na wanawake, nawanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao sadakawanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume nawanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingiwanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.
[33.37] Na ulipo mwambia yule Mwenyezi Mungu aliyemneemesha, nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo, namche Mwenyezi Mungu. Na ukaficha nafsini mwako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu,hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea.Basi Zaid alipo kwisha haja naye tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto waowa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shurutiza t'alaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.
[33.50] Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako ulio wapamahari yao, na ulio wamiliki kwa mkono wako wa kuliakatika alio kupa Mwenyezi Mungu, na mabinti ami zako,na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajombazako, na mabinti wa dada za mama yako walio hamapamoja nawe; na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwaNabii, kama mwenyewe Nabii akitaka kumwoa. Ni halalikwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Sisi tunajuatuliyo wafaridhia wao katika wake zao na wanawake iliowamiliki mikono yao ya kulia. Ili isiwe dhiki kwao. NaMwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[33.51] Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao,na umsogeze umtakaye. Na kama ukimtaka yule uliyemtenga, basi si vibaya kwako. Kufanya hivi kutapelekeayaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhijuu ya kile unacho wapa wao wote. Na Mwenyezi Munguanajua yaliyomo nyoyoni mwenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.
[33.53] Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ilampewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakinimtakapo itwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni,wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabiinaye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwajambo la haki. Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyozenu na nyoyo zao. Wala haikufalieni kumuudhi Mtume waMwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya MwenyeziMungu.
[33.55] Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na babazao, wala watoto wao, wala ndugu zao, wala watoto wandugu zao wanaume, wala watoto wa ndugu zao wanawake, wala wanawake wenzao, wala wale iliyo wamiliki mikonoyao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.