The Muslims Internet Directory
SURAT YA-SIN
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT YA-SIN
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[36.1] Ya-Sin (Y.S.).
[36.2] Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima!
[36.3] Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa,
[36.4] Juu ya Njia Iliyo Nyooka.
[36.5] Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
[36.6] Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basiwao wamekuwa wenye kughafilika.
[36.7] Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengikatika wao, kwa hivyo hawaamini.
[36.8] Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafikavidevuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu.
[36.9] Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao,na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni.
[36.10] Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye,hawataamini.
[36.11] Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, naakamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basimbashirie huyo msamaha na ujira mwema.
[36.12] Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandikawanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kilakitu tumekihifadhi katika daftari asli lenyekubainisha.
[36.13] Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikiawalio tumwa.
[36.14] Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basitukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema:Hakika sisi tumetumwa kwenu.
[36.15] Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kamasisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyimnasema uwongo tu.
[36.16] Wakasema: Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakikasisi tumetumwa kwenu.
[36.17] Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi.
[36.18] Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi.Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, namtapata adhabu chungu kutoka kwetu.
[36.19] Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwakuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukiamipaka.
[36.20] Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wamjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa.
[36.21] Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwawenyewe wameongoka.
[36.22] NA KWA NINI nisimuabudu yule aliye niumba na kwakemtarejeshwa?
[36.23] Je! Niishike miungu mingine badala yake?Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madharauombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa.
[36.24] Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu uliodhaahiri.
[36.25] Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basinisikilizeni!
[36.26] Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watuwangu wangeli jua
[36.27] Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, naakanifanya miongoni mwa walio hishimiwa.
[36.28] Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshikutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha.
[36.29] Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa!
[36.30] Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila waohumkejeli.
[36.31] Je! Hawaoni umma ngapi tulizo ziangamiza kablayao? Hakika hao hawarejei tena kwao.
[36.32] Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwembele yetu.
[36.33] Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasitukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawawanazila!
[36.34] Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende namizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake,
[36.35] Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa namikono yao! Basi je, hawashukuru?
[36.36] Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jikevyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsizao, na katika wasivyo vijua.
[36.37] Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana,mara wao wanakuwa gizani.
[36.38] Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo nimakadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.
[36.39] Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kamakarara kongwe.
[36.40] Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupitamchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.
[36.41] Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriyazao katika jahazi ilio sheheni.
[36.42] Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyo vipanda.
[36.43] Na tukitaka tunawazamisha, wala hapana wakuwasaidia, wala hawaokolewi,
[36.44] Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehekwa muda.
[36.45] Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenuna yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa...
[36.46] Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Molawao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza.
[36.47] Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeniMwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini:Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu uliodhaahiri.
[36.48] Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyini wakweli?
[36.49] Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukuanao wamo kuzozana.
[36.50] Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu waohawarejei.
[36.51] Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburiniwakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.
[36.52] Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenyemalazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehemana wakasema kweli Mitume.
[36.53] Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wotewatahudhuruishwa mbele yetu.
[36.54] Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, walahamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda.
[36.55] Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini,wamefurahi.
[36.56] Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juuya viti vya fakhari.
[36.57] Watapata humo kila namna ya matunda na watapatakila watakacho kitaka.
[36.58] "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola MleziMwenye kurehemu.
[36.59] Na enyi wakosefu! Jitengeni leo!
[36.60] Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwamsimuabudu Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahirikwenu.
[36.61] Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia IliyoNyooka.
[36.62] Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundikubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri?
[36.63] Hii basi ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa.
[36.64] Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.
[36.65] Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikonoyao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwawakiyachuma.
[36.66] Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali machoyao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje?
[36.67] Na tungeli taka tunge wageuza sura hapo hapowalipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi.
[36.68] Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo.Basi je! hawazingatii?
[36.69] Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, walahayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbushona Qur'ani inayo bainisha.
[36.70] Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu yamakafiri.
[36.71] Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawawenye kuwamiliki.
[36.72] Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wakowanao wapanda, na baadhi yao wanawala.
[36.73] Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je,hawashukuru?
[36.74] Na wameishika miungu mingine badala ya MwenyeziMungu ili ati wapate kusaidiwa!
[36.75] Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwaaskari wao watakao hudhurishwa.
[36.76] Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisitunayajua wanayo yaweka siri na wanayo yatangaza.
[36.77] Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumbayeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndioamekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri!
[36.78] Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake,akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayoimekwisha mung'unyika?
[36.79] Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo maraya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.
[36.80] Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wakijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.
[36.81] Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumbamfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi.
[36.82] Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu:Kuwa! Na kikawa.
[36.83] Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umoUfalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa.
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN