The Muslims Internet Directory
SURAT ASS'AFFAT
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT ASS'AFFAT
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[37.1] Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.
[37.2] Na kwa wenye kukataza mabaya.
[37.3] Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
[37.4] Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
[37.5] Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo katiyao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
[37.6] Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambola nyota.
[37.7] Na kulinda na kila shet'ani a'si.
[37.8] Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Nawanafukuzwa huko kila upande.
[37.9] Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
[37.10] Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na marahumfwatia kimondo kinacho ng'ara.
[37.11] Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi auhao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba waokwa udongo unao nata.
[37.12] Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
[37.13] Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.
[37.14] Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.
[37.15] Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu uliodhaahiri.
[37.16] Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndiokweli tutafufuliwa?
[37.17] Hata baba zetu wa zamani?
[37.18] Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
[37.19] Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndiowataona!
[37.20] Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
[37.21] Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwamkiikadhibisha.
[37.22] Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na haowalio kuwa wakiwaabudu -
[37.23] Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia yaJahannamu!
[37.24] Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:
[37.25] Mna nini? Mbona hamsaidiani?
[37.26] Bali hii leo, watasalimu amri.
[37.27] Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.
[37.28] Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujiaupande wa kulia.
[37.29] Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwaWaumini.
[37.30] Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyiwenyewe mlikuwa wapotovu.
[37.31] Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwishatuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.
[37.32] Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwawapotovu.
[37.33] Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikianakatika adhabu pamoja.
[37.34] Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.
[37.35] Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'LlahuHapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.
[37.36] Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwaajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?
[37.37] Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikishaMitume.
[37.38] Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabuchungu.
[37.39] Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
[37.40] Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
[37.41] Hao ndio watakao pata riziki maalumu,
[37.42] Matunda, nao watahishimiwa.
[37.43] Katika Bustani za neema.
[37.44] Wako juu ya viti wamekabiliana.
[37.45] Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji chachemchem
[37.46] Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.
[37.47] Hakina madhara, wala hakiwaleweshi.
[37.48] Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya stahamazuri.
[37.49] Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.
[37.50] Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.
[37.51] Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika miminalikuwa na rafiki
[37.52] Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanaosadiki
[37.53] Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndiotutalipwa na kuhisabiwa?
[37.54] Atasema: Je! Nyie mnawaona?
[37.55] Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.
[37.56] Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza.
[37.57] Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila yashaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa.
[37.58] Je! Sisi hatutakufa,
[37.59] Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisihatutaadhibiwa.
[37.60] Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.
[37.61] Kwa mfano wa haya nawatende watendao.
[37.62] Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti waZaqqum?
[37.63] Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwawalio dhulumu.
[37.64] Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu.
[37.65] Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vyamashet'ani.
[37.66] Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, nawajaze matumbo.
[37.67] Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa majiyamoto yaliyo chemka.
[37.68] Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwakwenye Jahannamu.
[37.69] Hakika waliwakuta baba zao wamepotea.
[37.70] Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.
[37.71] Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengiwa watu wa zamani.
[37.72] Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.
[37.73] Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa.
[37.74] Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
[37.75] Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wawaitikiaji.
[37.76] Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msibamkubwa.
[37.77] Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.
[37.78] Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kujabaadaye.
[37.79] Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!
[37.80] Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanyamema.
[37.81] Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
[37.82] Kisha tukawazamisha wale wengine.
[37.83] Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,
[37.84] Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.
[37.85] Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
[37.86] Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala yaMwenyezi Mungu?
[37.87] Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?
[37.88] Kisha akapiga jicho kutazama nyota.
[37.89] Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!
[37.90] Nao wakamwacha, wakampa kisogo.
[37.91] Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia:Mbona hamli?
[37.92] Mna nini hata hamsemi?
[37.93] Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.
[37.94] Basi wakamjia upesi upesi.
[37.95] Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichongawenyewe?
[37.96] Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyina hivyo mnavyo vifanya!
[37.97] Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motonihumo!
[37.98] Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakinitukawafanya wao ndio wa chini.
[37.99] Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Molawangu Mlezi; Yeye ataniongoa.
[37.100] Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongonimwa watenda mema.
[37.101] Basi tukambashiria mwana aliye mpole.
[37.102] Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamojanaye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeonausingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanaosubiri.
[37.103] Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlazajuu ya kipaji.
[37.104] Tulimwita: Ewe Ibrahim!
[37.105] Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyotunavyo walipa wanao tenda mema.
[37.106] Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.
[37.107] Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.
[37.108] Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kujabaadaye.
[37.109] Iwe salama kwa Ibrahim!
[37.110] Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
[37.111] Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
[37.112] Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabiimiongoni mwa watu wema.
[37.113] Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwadhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsizao waziwazi.
[37.114] Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.
[37.115] Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhikikubwa.
[37.116] Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenyekushinda.
[37.117] Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha.
[37.118] Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
[37.119] Na tukawaachia (sifa njema) katika watu waliokuja baadaye.
[37.120] Iwe salama kwa Musa na Haruni!
[37.121] Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
[37.122] Hakika wawili hao ni katika waja wetu walioamini.
[37.123] Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongonimwa Mitume.
[37.124] Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?
[37.125] Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,
[37.126] Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wababa zenu wa zamani?
[37.127] Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;
[37.128] Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
[37.129] Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kujabaadaye.
[37.130] Iwe salama kwa Ilyas.
[37.131] Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
[37.132] Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
[37.133] Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwaMitume.
[37.134] Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,
[37.135] Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma.
[37.136] Kisha tukawaangamiza wale wengineo.
[37.137] Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,
[37.138] Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?
[37.139] Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
[37.140] Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.
[37.141] Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katikawalio shindwa.
[37.142] Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
[37.143] Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasaMwenyezi Mungu,
[37.144] Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku yakufufuliwa.
[37.145] Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yumgonjwa.
[37.146] Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila yamung'unye.
[37.147] Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.
[37.148] Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
[37.149] Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenyewatoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?
[37.150] Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na waowakashuhudia?
[37.151] Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
[37.152] Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shakahao ni waongo!
[37.153] Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?
[37.154] Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
[37.155] Hamkumbuki?
[37.156] Au mnayo hoja iliyo wazi?
[37.157] Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
[37.158] Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake namajini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwawao watahudhurishwa.
[37.159] Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayowanayo msingizia.
[37.160] Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
[37.161] Basi hakika nyinyi na mnao waabudu
[37.162] Hamwezi kuwapoteza
[37.163] Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.
[37.164] Na hapana katika sisi ila anapo mahali pakemaalumu.
[37.165] Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangaosafu.
[37.166] Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.
[37.167] Na walikuwapo walio kuwa wakisema:
[37.168] Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,
[37.169] Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa MwenyeziMungu wenye ikhlasi.
[37.170] Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.
[37.171] Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tanguliakwa waja wetu walio tumwa.
[37.172] Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.
[37.173] Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.
[37.174] Basi waachilie mbali kwa muda.
[37.175] Na watazame, nao wataona.
[37.176] Je! Wanaihimiza adhabu yetu?
[37.177] Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhimbaya kwa walio onywa.
[37.178] Na waache kwa muda.
[37.179] Na tazama, na wao wataona.
[37.180] Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola MleziMwenye enzi na yale wanayo mzulia.
[37.181] Na Salamu juu ya Mitume.
[37.182] Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu MolaMlezi wa walimwengu wote.
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN