[38.24] Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoowako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakikawashirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. NaDaudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwombamsamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia.