[39.6] Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanyamwenziwe katika nafsi ile ile. Na akakuleteeni wanyamawa mifugo jozi nane. Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu.Huyu ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme niwake. Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?
[39.7] Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi,lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuruYeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi.Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeyeni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani.
[39.8] Na taabu inapo mfikia mtu humwomba Mola wake Mlezinaye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake,husahau yale aliyo kuwa akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watunjia yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa mudamchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watuwa Motoni.
[39.21] Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha majikutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchemkatika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali? Kisha hunyauka ukaionaimekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila yashaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili.
[39.23] Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa,Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwachongozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka MwenyeziMungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huohumwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa.
[39.38] Na ukiwauliza: Ni nani aliye ziumba mbingu naardhi. Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema:Je! Mnawaonaje wale mnao waomba badala ya MwenyeziMungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, waowanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitakakunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema:Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye wategemeewanao tegemea.
[39.71] Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwamakundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milangoyake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeniAya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa sikuyenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri.