
[4.23] Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dadazenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wandugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wawake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinziwenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Piammeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katikamigongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu niMwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
|