[42.14] Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia ilimu kwasababu ya husuda iliyo kuwa baina yao. Na lau kuwahaikwisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya kuakhirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shakapalingeli hukumiwa baina yao. Na hakika waliorithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayo wahangaisha.
[42.15] Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kamaulivyo amrishwa, wala usiyafuate matamanio yao. Nasema: Naamini aliyo teremsha Mwenyezi Mungu katika Vitabu. Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu.Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na Mola wenu Mlezi.Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu, na nyinyi mna jukumu kwa vitendo vyenu. Hapana kuhojiana baina yetuna nyinyi. Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, namarejeo ni kwake.