[46.15] Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazaziwake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu,na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapofika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini,husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitendemema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu.Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.
[46.17] Na ambaye amewafyonya wazazi wake na akawaambia:Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazivingi vimekwisha pita kabla yangu! Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu (na humwambia mtotowao): Ole wako! Amini! Hakika ahadi ya Mwenyezi Munguni kweli. Na yeye husema: Hayakuwa haya ila ni visavya watu wa kale.
[46.26] Na bila ya shaka tuliwaweka vizuri sio kamatulivyo kuwekeni nyinyi; na tuliwapa masikio, namacho, na nyoyo. Na hayakuwafaa kitu masikio yao, walamacho yao, wala nyoyo zao kwa lolote. Kwani haowalikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yalewaliyo kuwa wakiyafanyia maskhara ndiyo yakawazunguka.