[48.11] Watakuambia mabedui walio baki nyuma:Yametushughulisha mali yetu na ahali zetu, basituombee msamaha. Wanasema kwa ndimi zao yasiyo kuwamokatika nyoyo zao. Sema: Ni nani awezaye kukusaidienichochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kukudhuruni au akitaka kukunufaisheni? Bali MwenyeziMungu anazo khabari za mnayo yatenda.
[48.25] Hao ndio walio kufuru na wakakuzuieni msiingieMsikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu kufikamahala pao. Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msio wajua mkawasaga na mkaingia makosanikutokana nao bila ya kujua ...Mwenyezi Mungu (amefanyahaya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake. Lau wangeli tengana bila ya shaka tungeli waadhibu waliokufuru kwa adhabu chungu.
[48.29] Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na waliopamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, nawanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama nakusujudu wakitafuta fadhila na radhi za MwenyeziMungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katikaTaurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene,ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahishawakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri.Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatendamema katika wao msamaha na ujira mkubwa.