
[5.3] Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama yanguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili yaMwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, naaliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, naaliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama,ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyamaaliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli.Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaana Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi.Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizienineema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyoDini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu niMsamehevu na Mwenye kurehemu.
|