The Muslims Internet Directory
SURAT ADH-DHAARIYAAT
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Library ↓
Prayer Times
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Classifieds ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
More... ↓
Login/Register
Muslims Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Islamic Classifieds
WebRing Sites
Help/FAQ
Help?
-
Live!
Advertisement
:
Featured Site
Feature Your Site Now
Paid Services
Buy The Islamic CD
Banner Design
Submit Your Site
Muslims Million Pixels
2Muslims Services
Free E-mail Account
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
New
Free Guestbook
New
Islamic Internet Gadgets
Prayer Times Software
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Polls and Votting
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Holidays Dates
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
How To Pray?
Translate Site To:
Arabic
Bulgarian
Catalan
Chinese (Simplified)
Chinese (Traditional)
Croatian
Czech
Danish
Dutch
English
Filipino
Finnish
French
German
Greek
Hebrew
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latvian
Lithuanian
Norwegian
Polish
Portuguese
Romanian
Russian
Serbian
Slovak
Slovenian
Spanish
Swedish
Ukrainian
Vietnamese
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
view results
view other polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: SURAT ADH-DHAARIYAAT
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Chinese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[51.1] Naapa kwa pepo zinazo tawanya,
[51.2] Na zinazo beba mizigo,
[51.3] Na zinazo kwenda kwa wepesi.
[51.4] Na zinazo gawanya kwa amri,
[51.5] Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli,
[51.6] Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
[51.7] Naapa kwa mbingu zenye njia,
[51.8] Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayokhitalifiana.
[51.9] Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
[51.10] Wazushi wameangamizwa.
[51.11] Ambao wameghafilika katika ujinga.
[51.12] Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
[51.13] Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni.
[51.14] Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwamkiyahimiza.
[51.15] Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani nachemchem.
[51.16] Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakikahao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
[51.17] Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.
[51.18] Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.
[51.19] Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba naasiye omba.
[51.20] Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
[51.21] Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?
[51.22] Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyoahidiwa.
[51.23] Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi,hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyimnasema.
[51.24] Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaohishimiwa?
[51.25] Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeyeakasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.
[51.26] Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliyenona.
[51.27] Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
[51.28] Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema:Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenyeilimu.
[51.29] Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema naakijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi nikikongwe na tasa!
[51.30] Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wakoMlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.
[51.31] AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mliotumwa?
[51.32] Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,
[51.33] Tuwatupie mawe ya udongo,
[51.34] Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwaajili ya wanao pindukia mipaka.
[51.35] Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.
[51.36] Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenyeWaislamu!
[51.37] Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopaadhabu chungu.
[51.38] Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwaFirauni na hoja wazi.
[51.39] Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake naakasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
[51.40] Basi tukamkamata yeye na majeshi yake natukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
[51.41] Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepowa kukata uzazi.
[51.42] Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanyakama kilio nyambuka.
[51.43] Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa:Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.
[51.44] Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakuamoto wa radi nao wanaona.
[51.45] Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenyekujitetea.
[51.46] Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwawatu wapotovu.
[51.47] Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakikaSisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.
[51.48] Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazurinamna gani Sisi!
[51.49] Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ilimzingatie.
[51.50] Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
[51.51] Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja naMwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wakubainisha nitokae kwake.
[51.52] Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtumeila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.
[51.53] Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watuwaasi.
[51.54] Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.
[51.55] Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
[51.56] Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.
[51.57] Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.
[51.58] Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku,Mwenye nguvu, Madhubuti.
[51.59] Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kamafungu la wenzao. Basi wasinihimize.
[51.60] Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa.
Featured Ad
About Us
Contact Us
Advertise
Donate/Support
Sign Guestbook
Link To Us
Newsletter
Recommend
What's New
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Pharmacy Site
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2009
Islamic Education & Services Institute