[53.32] Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendovichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wakoMlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifuusafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.