The Muslims Internet Directory
SURAT ARRAH'MAN
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT ARRAH'MAN
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[55.1] Arrah'man, Mwingi wa Rehema
[55.2] Amefundisha Qur'ani.
[55.3] Amemuumba mwanaadamu,
[55.4] Akamfundisha kubaini.
[55.5] Jua na mwezi huenda kwa hisabu.
[55.6] Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
[55.7] Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani,
[55.8] Ili msidhulumu katika mizani.
[55.9] Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katikamizani.
[55.10] Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
[55.11] Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
[55.12] Na nafaka zenye makapi, na rehani.
[55.13] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha
[55.14] Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
[55.15] Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
[55.16] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha
[55.17] Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibimbili.
[55.18] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.19] Anaziendesha bahari mbili zikutane;
[55.20] Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
[55.21] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.22] Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu namarijani.
[55.23] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.24] Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyoundwa kama vilima.
[55.25] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.26] Kila kilioko juu yake kitatoweka.
[55.27] Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenyeutukufu na ukarimu.
[55.28] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.29] Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi.Kila siku Yeye yumo katika mambo.
[55.30] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.31] Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
[55.32] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.33] Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenyakwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ilakwa kupewa madaraka.
[55.34] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.35] Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; walahamtashinda.
[55.36] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.37] Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
[55.38] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.39] Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
[55.40] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.41] Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basiwatashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
[55.42] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.43] Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
[55.44] Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya motoyanayo chemka.
[55.45] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.46] Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wakeMlezi atapata Bustani mbili.
[55.47] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.48] Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
[55.49] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.50] Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
[55.51] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.52] Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
[55.53] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.54] Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya haririnzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
[55.55] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.56] Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao;hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
[55.57] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.58] Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
[55.59] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha.
[55.60] Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
[55.61] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.62] Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
[55.63] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.64] Za kijani kibivu.
[55.65] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.66] Na chemchem mbili zinazo furika.
[55.67] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.68] Imo humo miti ya matunda, na mitende namikomamanga.
[55.69] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.70] Humo wamo wanawake wema wazuri.
[55.71] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.72] Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
[55.73] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.74] Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
[55.75] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.76] Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazuliamazuri.
[55.77] Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
[55.78] Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufuna ukarimu.
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN