The Muslims Internet Directory
SURAT AL-WAAQIA'H
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT AL-WAAQIA'H
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[56.1] Litakapo tukia hilo Tukio
[56.2] Hapana cha kukanusha kutukia kwake.
[56.3] Literemshalo linyanyualo,
[56.4] Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso,
[56.5] Na milima itapo sagwasagwa,
[56.6] Iwe mavumbi yanayo peperushwa,
[56.7] Na nyinyi mtakuwa namna tatu:-
[56.8] Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?
[56.9] Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?
[56.10] Na wa mbele watakuwa mbele.
[56.11] Hao ndio watakao karibishwa
[56.12] Katika Bustani zenye neema.
[56.13] Fungu kubwa katika wa mwanzo,
[56.14] Na wachache katika wa mwisho.
[56.15] Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa.
[56.16] Wakiviegemea wakielekeana.
[56.17] Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele,
[56.18] Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywajikutoka chemchem safi.
[56.19] Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo walahawatoleweshwa.
[56.20] Na matunda wayapendayo,
[56.21] Na nyama za ndege kama wanavyo tamani.
[56.22] Na Mahurulaini,
[56.23] Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa.
[56.24] Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
[56.25] Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi,
[56.26] Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama.
[56.27] Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wakuliani?
[56.28] Katika mikunazi isiyo na miba,
[56.29] Na migombailiyo pangiliwa,
[56.30] Na kivuli kilicho tanda.
[56.31] Na maji yanayo miminika,
[56.32] Na matunda mengi,
[56.33] Hayatindikii wala hayakatazwi,
[56.34] Na matandiko yaliyo nyanyuliwa.
[56.35] Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya,
[56.36] Na tutawafanya vijana,
[56.37] Wanapendana na waume zao, hirimu moja.
[56.38] Kwa ajili ya watu wa kuliani.
[56.39] Fungu kubwa katika wa mwanzo,
[56.40] Na fungu kubwa katika wa mwisho. 3
[56.41] Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
[56.42] Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka,
[56.43] Na kivuli cha moshi mweusi,
[56.44] Si cha kuburudisha wala kustarehesha.
[56.45] Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maishaya anasa.
[56.46] Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa,
[56.47] Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawaudongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?
[56.48] Au baba zetu wa zamani?
[56.49] Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho
[56.50] Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa sikumaalumu.
[56.51] Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha,
[56.52] Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.
[56.53] Na kwa mti huo mtajaza matumbo.
[56.54] Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka.
[56.55] Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenyekiu.
[56.56] Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo.
[56.57] Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
[56.58] Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?
[56.59] Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
[56.60] Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
[56.61] Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyikwa umbo msilo lijua.
[56.62] Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza,basi kwa nini hamkumbuki?
[56.63] Je! Mnaona makulima mnayo yapanda?
[56.64] Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenyekuotesha?
[56.65] Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe,mkabaki mnastaajabu,
[56.66] Mkisema: Hakika sisi tumegharimika;
[56.67] Bali sisi tumenyimwa.
[56.68] Je! Mnayaona maji mnayo yanywa?
[56.69] Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni auni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
[56.70] Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basimbona hamshukuru?
[56.71] Je! Mnauona moto mnao uwasha?
[56.72] Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndioWaumbaji?
[56.73] Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwawalioko nyikani.
[56.74] Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
[56.75] Basi naapa kwa maanguko ya nyota,
[56.76] Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa,laiti mngeli jua!
[56.77] Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,
[56.78] Katika Kitabu kilicho hifadhiwa.
[56.79] Hapana akigusaye ila walio takaswa.
[56.80] Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wawalimwengu wote.
[56.81] Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?
[56.82] Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanyakuwa mnakadhibisha?
[56.83] Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,
[56.84] Na nyinyi wakati huo mnatazama!
[56.85] Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.
[56.86] Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
[56.87] Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyimnasema kweli?
[56.88] Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,
[56.89] Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
[56.90] Na akiwa katika watu wa upande wa kulia,
[56.91] Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu waupande wa kulia.
[56.92] Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
[56.93] Basi karamu yake ni maji yanayo chemka,
[56.94] Na kutiwa Motoni.
[56.95] Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.
[56.96] Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliyeMkubwa.
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN