[59.2] Yeye ndiye aliye watoa walio kufuru miongoni mwaWatu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa uhamisho wakwanza. Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu. LakiniMwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipo patazamia,na akatia woga katika nyoyo zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini. Basizingatieni enyi wenye macho!

[59.7] Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wakekutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili yaMwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, namayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiweyakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
