[6.19] Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema:Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu nanyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kwelinyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapomiungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema:Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnaowashirikisha.
[6.70] Waachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo napumbao, na uhai wa dunia ukawaghuri. Nawe kumbushakwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyo yachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila MwenyeziMungu. Na ingatoa kila fidia haitokubaliwa. Hao ndiowalio angamizwa kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, naadhabu chungu.
[6.71] Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambaehatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada yaMwenyezi Mungu kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet'ani wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anaomarafiki wanao mwita ende kwenye uwongofu,wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu waMwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwatusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote,
[6.91] Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadriyake, walipo sema: Mwenyezi Mungu hakumteremshiamwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyo teremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofukwa watu, mlicho kifanya kurasa kurasa mkizionyesha,na mengi mkiyaficha. Na mkafunzwa mlio kuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: Mwenyezi Mungu. Kishawaache wacheze katika porojo lao.
[6.93] Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliyauwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewawahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha MwenyeziMungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwakatika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu!Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake.
[6.99] Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni;na kwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kutokana nabaadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yakepunje zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatokakwenye makole yake mashada yaliyo inama; na bustani zamizabibu na mizaituni, na makomamanga, yaliyo fanana na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa nayakawiva. Hakika katika hayo pana Ishara kwa watuwanao amini.
[6.124] Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoaminimpaka tupewe mfano wa walio pewa Mitume wa MwenyeziMungu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujuawapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia hao walio kosaudhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwasababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.
[6.128] Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyimakundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasiwengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisina wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. BasiMwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. HakikaMola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua.
[6.136] Na wamemwekea sehemu Mwenyezi Mungu katika mimeana wanyama alio umba, nao husema: Hii ni sehemu yaMwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miunguyao havimfikii Mwenyezi Mungu, na vilivyo kuwa vyaMwenyezi Mungu huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu.
[6.141] Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaajuu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimeayenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kulenimatunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku yakuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.
[6.144]Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe.Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majikewawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya?Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzuliaMwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidiwatu madhaalimu.
[6.145] Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitukilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ninyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofukimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu.Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamaniwala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi niMwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[6.146] Na wale walio fuata dini ya Kiyahuditumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharimishiashahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao aumatumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisindio wasema kweli.
[6.148] Watasema walio shirikisha: Lau kuwa MwenyeziMungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala babazetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivihivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipoonja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimumtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ilauwongo tu.
[6.151] Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieniMola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye nachochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisitunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambomachafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Walamsiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimishakuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ilimyatie akilini.
[6.152] Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia yawema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizenivipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtuila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwauadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Munguitekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka.
[6.157] Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabutungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basiimekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, nauwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwazaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipawanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwasababu ya kujitenga kwao.
[6.158] Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, auawafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Isharaza Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi yaIshara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtukitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanyakheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja.