[60.1] Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenukuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwishaikataa haki iliyo kujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu, MolaMlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njiayangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayo yaficha na mnayodhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basiameipotea njia ya sawa.
[60.4] Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim nawale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao:Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; naumekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyimpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakikanitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajiliyako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndiomarejeo.
[60.10] Enyi mlio amini! Wakikujilieni wanawake Wauminiwalio hama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungundiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajuakuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri.Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala haomakafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni haowanaume mahari walio toa. Wala hapana makosa kwenukuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawakemakafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Na takenimlicho kitoa, na wao watake walicho kitoa. Hiyo ndiyohukumu ya Mwenyezi Mungu anayo kuhukumuni. Na MwenyeziMungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.
[60.12] Ewe Nabii! Watakapo kujia wanawake Wauminiwanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Munguna chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushiwanao uzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguuyao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peananao ahadi, na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi maghfira, Mwenyekurehemu.